Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu Wa shirika la utangazaji nchini TBC, Tido Muhando, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi.
Mhando anakabiliwa na mashtaka manne ya matumizi mabaya ya madaraka na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887 milioni wakati akiwa mkurugenzi TBC.
Hata hivyo mkurugenzi huyo ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti matatu ya dhamana, katika mashtaka matano yanayomkabili ya matumizi mabaya ya madaraka