Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 27.11.2018: Wenger, Cahill, Ibrahimovic, Arnautovic, Witsel, Pulisic - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


nuru+ya+habar

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Tuesday, November 27, 2018

demo-image

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 27.11.2018: Wenger, Cahill, Ibrahimovic, Arnautovic, Witsel, Pulisic

Responsive Ads Here
HABARI KUU Sambaza habari hii Messenge
_104504617_gettyimages-958369646-1Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionArsene Wenger
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anataka kurejea kwenye usimamizi wa kandanda huko Bayern Munich ambao wanamuona Mfaransa huyo kama mrithi wa Nico Kovac. (Telegraph)
AC Milan wamekataa fursa ya kumsaini beki wa Chelsea na England Garry Cahil, 32. (Calciomercato, via Talksport)
Meneja wa AC Milan Gennaro Gattuso hajakana uwezekano wa kumsaini aliyekuwa mshambuliaji wa LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic, 37. (Sun)
Mshambualia wa Ubelgiji Eden Hazard, 27, anasema Chelsea wanalenga nafasi nne za kwanza msimu huu na hawatakuwa mabingwa. (Manchester Evening News)
_104504619_gettyimages-1071845452-1Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionEden Hazard
Manchester United wanataka kumsaini mshambuliaji wa West Ham na Austria Marko Arnautovic, 29. (Telegraph)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amefufua mikakati zake kumwinda mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Ubelgiji Axel Witsel. (ESPN)
_104504621_gettyimages-958102580Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDavid Moyes
Meneja wa zamani wa Manchester United David Moyes anaamini angepewa muda zaidi huko Old Traffor. (Talksport)
Borussia Dortmund wanajiandaa kumuuza wing'a Mmarekani Christian Pulisic kwenda Chelsea au Liverpool kwa pauni milioni 70 ikiwa mchezaji huyo wa miaka 20 atakaa Ujerumani hadi msimu ujao. (Telegraph)
_104504623_gettyimages-1059945856Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDeclan Rice
West Ham wanajiandaa kusubiri hadi msimu ujao kabla ya kuanza mazungumzo ya mkataba na mlinzi raia wa Jamhuri ya Ireland Declan Rice, 19. (Guardian)
Mchezaji wa kimataifa raia wa England Peter Beardsley anafunza klabu isiyo katika Ligi ya Gateshead kufuatia kutimuliwa kwake kama naibu meneja wa Newcastle mwezi January. (Mail)
_104504625_gettyimages-1054130936Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTanguy Ndombele
Everton wanammezea mate kiungo wa kati wa Lyon Mfaransa Tanguy Ndombele, 21, lakini anakabiliwa na ushindani kutoka Manchester City. (Liverpool Echo)
Arsenal wanamwinda beki wa Galatasaray Ozan Kabak lakini mchezaji huyo wa miaka 18 pia anawindwa na Inter Milan. (Sabah, via Talksport)
_104504657_gettyimages-1058405944Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionOzan Kabak
Klabu ya Serie A wanataka kumsaini beki wa Chelsea Mnigeria Ola Aina kwa mkataba wa kudumu baada ya kufurahishwa na mchezaji huyo tangu awasili kwa mkopo msimu huu. (Goal)
Inter Milan wanaripotiwa kutoa ofa kwa kwa mlinzi wa Manchester City na Ufaransa Eliaquim Mangala, 27. (Football Italia, via Talksport)

Bora Kutoka Jumatatu

_104504661_88822b6f-44b7-4088-a6d4-36d625d43108Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionOusmane Dembele
Mshambuliaji Mfaransa Ousmane Dembele, 21, ameomba kuondoka Barcelona mwezi Januari na kuondoka kwake kutamruhusu Neymar kurudi Nou Camp kutoka Paris St-Germain. (Goal)
Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 27 amekana kuwa atahamia Paris St-Germain, lakini amekiri kuwa ataondoka Stamford Bridge msimu huu. (Canal+ via Goal)
Mkurugenzi wa Milan Leonardo ameripotiwa kuwa kwenye mazungumzo na Chelsea kuhusu kiungo wa kati Cesc Fabregas, 31, na walinzi Gary Cahill, 32, na Andreas Christensen, 22. (Football Italia)
_104504662_c9dbe23d-c211-46b8-aeda-7c7715a0bc19Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionLorenzo Pellegrini
Manchester United ilituma maajenti kumtazama kijana mlinzi wa West Ham Declan Rice, 19, wakati Hammers walishindwa kwa mabao 4-0 na Manchester City siku ya Jumamosi. (Metro)
Beki wa Barcelona Jordi Alba, 29, amekiri kuwa hajapewa mkataba mpya klabuni na kuacha hatma yake gizani. (ESPN)
Manchester United wanaweza kungoja kumsaini kiungo wa kati wa Roma Lorenzo Pellegrini baada ya kugundua kuwa kupengee cha kuuvunja mkataba wake kinaweza kutumiwa mwisho wa msimu. (Mirror via Manchester Evening News)

Post Bottom Ad

HABARI

undefined

Contact Form

Name

Email *

Message *