- NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, May 31, 2018

HABARI KUU
DUMU 11 zinazosadikiwa kuwa ni Pombe haramu aina ya Gongo zimekamatwa katika Shehia ya Kiuyu Kipangani, Wilaya ya Micheweni zikiwa zimefukiwa ardhini baada ya kufanyika kwa Oparesheni ya kupambana na dawa za kulevya Wilayani hapa.

Kwa mjibu wa taarifa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bi Salama Mbarouk Khatib amesema kuwa katika oparesheni hiyo pia wamefanikiwa kukamata tangi moja la Maloweko yaliyokuwa yanaandaliwa kwa ajili ya kutengenezea Pombe hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Bi. Salama Mbarouk Khatib akishiriki zoezi la Ufukuaji wa Madumu ya Maloweko ambayo yamekutwa yamefichwa Ardhini wakati wa Oparesheni hiyo
Aidha Salama amewataka wananchi kuendelea kutoa mashirikiano kwa Jeshi la Polisi pamoja na Polisi jamii pindi wanapoona viashiriavya matendo hayo katika jamii zao ili kuhakikisha Pombe hizo zinatokomezwa.

Kwa mjibu wa Mkuu wa Wilaya hiyo watuhumiwa wawili wamekamatwa katika Oparesheni ambao ni Hamad Rashid Ali (23), Mkaazi wa Kipange pamoja mwenzake aliyefahamika kwa jina moja la Paulo na tayari wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi.

Madumu yaliyokamatwa katika oparesheni yakishishwa kituo cha Polisi Matangatuani. 
Oparesheni hiyo ya kupambana na Dawa za kulevya Wilaya ya Micheweni ni mwendelezo wa oparesheni inayoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambae pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bi Salama Mbarouk Khatib kwa kushirikiana na Polisi Jamii.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI