Chelsea 'wanaelekea kucheza Europa League' baada ya sare na West Ham - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, April 09, 2018

Chelsea 'wanaelekea kucheza Europa League' baada ya sare na West Ham

HABARI KUUMlinzi wa timu ya Chelsea Cesar AzpilicuetMlinzi wa timu ya Chelsea Cesar Azpilicueta anaamini kushinda FA hakutabadilisha hali kwamba umekuwa msimu mbaya
Kushinda kombe la FA hakutatosha "kunusuru" msimu wa klabu ya Chelsea, kwa mujibu wa beki wa klabu hiyo Cesar Azpilicueta.
Amesema hayo huku ikionekana wazi kwamba itakuwa mwujiza kwao kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.
Hii ni baada yao kutoka sare ya 1-1 West Ham na hivyo kudidimiza zaidi matumaini ya klabu hiyo kumaliza katika nafasi nne za kwanza Ligi Kuu ya England msimu huu.
Kutoka sare kwa timu hiyo Jumapili kumeiacha Chelsea ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi ya Premia wakiwa pointi 10 nyuma ya Liverpool na Tottenham katika nafasi ya tatu na ya nne.
Bao la kusawazisha la Javier Hernandez la kipindi cha nusu ya pili ya mchezo liliinua matarajio ya West Ham ya kuendelea kubakia katika michuano ya Ligi ya Premia dakika ya 73 lakini likawaumbua Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge.
Cesar AzpilicuetaCesar Azpilicueta aliifungia Chelsea bao lake la tano la Ligi ya Premia dhidi ya West Ham akicheza mechi yake ya 191
Inamaanisha kuwa huenda wasifuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.
"Tuko nyuma sana," alisema Azpilicueta, aliyekuwa amefungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 36.
''Ni kauli kubwa na kwa kiasi fulani aliyoitoa Azpilicueta... nimeipenda, anajivunia klabu yake na anafahamu fika malengo ya Chealsea, na kutoa kauli hiyo inamaanisha kuwa amevunjika moyo kwa mahala walipo sasa,'' alisema mchanganuzi wa mechi za siku Jermaine Jenas katika mazungumzo na BBC.Kocha wa timu ya Chelsea- Antonio ConteMustakabali wa kocha wa sasa wa Chelsea Antonio Conte haueleweki baada ya timu yake kuteteleka katika msimu huu wa Ligi ya Premia
Meneja wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho alifutwa kazi wakati wa msimu wa mwaka 2015-16, wakati timu hiyo ilipomaliza ikiwa katika nafasi ya 10 katika Ligi ya Premia.
Na maswali pia yanaibuka juu ya mustakabali wa kocha wa sasa Antonio Conte, ambaye ameongoza timu hiyo baada ya kushinda taji mwaka jana.
Huku zikiwa zimesalia mechi sita, kihesabu Chelsea inaweza kufika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, ingawa itabidi timu za Liverpool (ambao wamesalia na mechi tano) na Tottenham (ambao bado wana mechi sita za kucheza) ziporomoke.Javier Hernandez mchezaji wa timu ya West HamBao la kusawazisha la Javier Hernandez la kipindi cha nusu ya pili ya mchezo liliinua matarajio ya West Ham ya kuendelea kubakia katika michuano ya Ligi ya PrimiaLakini hata kama wataweza kusonga mbele na kushinda Kombe la FA halitakuwa liwazo kamili machoni mwa Azpilicueta, 28.
"Kombe la FA ni kombe kubwa lenye historia kubwa lakini halitoshi kwetu," mchezaji wa safu ya ulinzi wa timu ya taifa ya Uhispania aliambia BBC.
" Tutajaribu kulishinda lakini kombe halitunusuru kwenye msimu," aliongeza.
Azpilicueta, ambaye goli lake la kipindi cha kwanza cha mchezo wa Jumapili lilifutwa na goli za kusawazisha la Javier Hernandez katika kipindi cha pili aliongeza: "Kupata sare nyumbani katika uwanja mwingine wa London ni suala linaloleta mfadhaiko kwetu sote na kwa mashabiki wetu. Hatujafurahi.''
"Cha maana ni matokeo ya mwisho ya mechi, nimesikitika sana leo. Tulifaa kushinda mechi hii."
"Tulidhibiti mechi , tulikuwa na fursa za kutosha kushinda lakini tulihangaika hadi mwisho na labda wangeweza kushinda.
Imekuwa vigumu sana tena sana kwa kila mchezo unaochezwa."

Nyota wa mchezoEden HazardEden Hazard alikuwa mgumu kumkabili kwa upande wa Chelsea, huku akitoa fursa kwa wenyeji kufunga kwa timu hiyo iliyokuwa mwenyeji kabla ya nusu fainali'

Mechi inaakisi msimu wa Chelsea'

Meneja wa Chelsea Antonio Conte alisema: "Nadhani kwa mchezo huu tunaweza kuuona msimu wetu. Tunaweza kubuni fursa nyingi lakini hatuwezi kuzichukua.
"Sisi hatukutumia vyema naafsi za kufunga, kisha tunashambuliwa mara mbili kwa makombora yanayolenga goli na moja linakuwa bao.
"Kama haufungi lakini unaunda nafasi za kufunga ni vigumu sana kushinda. Mechi hii inaelezea msimu wetu."
Kuhusu kutojiamini, Conte alisema "Morata alifunga magoli mawili lakini yakakataliwa kwa sababu ya kuotea. Anajiamini na tulitoa fursa za kutosha kwa Hazard, Willian na Morata kufunga. Lakini ninarudia, mechi hii inaelezea msimu wetu."Meneja wa West Ham David MoyesMeneja wa West Ham David Moyes hakufurahishwa na bao la kona walilochapwa na ChelseaKwa upande wake meneja wa West Ham David Moyes alisema: "Ni alama muhimu sana kwetu. Tulikuwa tunacheza dhidi ya timu ambayo ina wachezaji wenye thamani na wenye mashambulio makali waliocheza vizuri."
"La muhimu lilikuwa ni kwamba hatukuwa nje ya mchezo wakati wote, kwa sababu namna walivyopata bao lao la kwanza ilikuwa ni jambo la kimiujiza. Chelsea wanaweza kupata bao kwa njia nyingine lakini kufunga kwa njia ya kona lilikuwa ni jambo baya kwa mtazamo wetu ."
Kwa mchezaji aliyeingia kama nguvu mpya Javier Hernandez kufunga bao la kusawazisha, Moyes alisema: "Chicharito hawezi kunishukuru kwa kumuingiza uwanjani kama mchezaji wa nguvu mpya, lakini ni mshambuliaji mzuri sana eneo la hatari na kila mara hufunga magoli.
"Kila mara unapotoa fursa kwa Chelsea huwa inakuwa hatari kidogo, lakini kwa ujumla tulijilinda vizuri dhidi yao," alisema Moyes.
Chelsea itakabiliana na Southampton Jumapili katika mchuano wa wao wa nusu fainali ya Kombe la FA katika uwanja wa Wembley.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI