Michuano ya fainali ya soka la ufukweni inatarajiwa kuanza Disemba 8 hadi 14 mwaka huu katika mji wa Sharm El Sheikh nchini Misri.Timu ya taifa ya soka la ufukweni ya Tanzania, imetua salama nchini humo baada ya kuondoka jana alfajiri kwenda nchini humo kuiwakilisha Tanzania baada ya kuibuka kidedea katika michuano ya Copa Dar es salaam yaliyomalizika hivi karibuni nchini Tanzania.
Kundi A lina timu za Misri, Morocco, Ivory Coast na Madagascar wakati kundi B lina timu toka Tanzania, mabingwa watetezi Senegal, Nigeria na Libya.
Tanzania itafungua dimba siku ya jumamosi kwa kukutana na Libya, kabla ya kumenyana na Senegal jumapili na kumalizia na Nigeria siku ya jumatatu.