Millioni 240 zatumika kuinua mradi wa uvuvi Zanzibar - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, November 13, 2018

Millioni 240 zatumika kuinua mradi wa uvuvi Zanzibar

HABARI KUU
Wanakijiji wa Paje wakikabidhiwa boti maalum ya uvuvi na shirika la Direct Aid.
Jumla ya Tsh Millioni mia mbili na Arobaini zinatatumika kufanikisha miradi ya uvuvi kwenye vijiji mbali mbali kwa lengo la kusaidia vijiji hivyo.
Akizugumza na muandishi wetu, Mkuregenzi wa Shirika la Direct Aid Aiman Mohamed Kamal Din amesema shirika lake limeamua kusaidia jamii hususan kwa baadhi ya vijiji kwa mwaka huu 2018 kwenye maeneo ya uvuvi ikiwemo kukabidhiwa boti maalum za kisasa kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.
Aiman Mohamedi amevitaja vijiji hivyo ni Uzi, Bumbwini, Tumbatu na Paje kwa upande wa Unguja na baadhi ya maeneo kisiwani Pemba kwa lengo la kuwezesha kujingizia kipato cha kila siku.
Amesema boti hizo zitaendana na vifaa vya kisasa na miradi hiyo hupewa bure bila ya mikopo ili kuwezesha wananchi wa Zanzibar kwa wale ambao wanatatizo la ajira vijijini.
Kwa upande wake Mwakilishi wa jimbo la Bumbwini wakati wa ukabidhi wa boti moja ndani ya kijiji chake Mkoa wa Kaskazini unguja Bi Mtumwa Pea Yussufu amelipongeza Shirika hilo la Direct Aid kwa bidii yake baada ya kukabidhi boti moja kwa madrasa ‘’ Khairiya Islamiya’’ iliyokuwepo kitongoji cha Bumbwi Baga .
Amesem boti hiyo inaweza kusaidia tatizo la ajira na kujipatia kipato na kuendeleza madrasa hiyo ili kutoa muamko kwa walimu wa madrasa hiyo kuweza kundelea kimaendeleo.
Amewaomba wenye madrasa hiyo kuweza kukitunza chombo hicho ili kuweza kuzalisha chombo chengine kama hicho kuweza kuwasaidia kama mradi ndani ya madrasa hiyo.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI