
Kombe la Shirikisho barani Afrika: Mtibwa kuanza kupeperusha bendera ya Tanzania
Kikosi cha Mtibwa Sugar, leo kitakuwa uwanjani kupeperusha bendera ya Tanzania katika mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Northern Dynamos ya Shelisheli utakaochezwa uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Kocha mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema ana imani na kikosi chake licha ya kutokuwa na wachezaji wa kigeni kutokana na mafunzo ambayo amewapa.
Tanzania inawakilishwa na timu mbili kimataifa ambapo kwenye kombe la Shirikisho ni Mtibwa na kwa upande wa kombe la mabingwa la Afrika ni Simba ambao watacheza na Mbabane Swallows FC kutoka Swaziland kesho.