Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza
na wananchi wa Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi
akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018.
Mhandisi Joseph Mwakabage Meneja Mradi wa Mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe (Aliyenyoosha mkono) akimuonyeshaNaibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko mitambo ya uchimbaji madini alipotembelea mgodi huo uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua eneo la uchimbaji madini ya makaa ya mawe alipotembelea mgodi wa Edenville Tanzania Ltd uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018.
Mhandisi Joseph Mwakabage Meneja Mradi wa Mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe (Kulia) akimueleza Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko juu ya uchimbaji wa makaa ya mawe alipotembelea mgodi huo uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, 23 Februari 2018.
Na Mathias Canal, Rukwa
Serikali imesema kuwa sheria mpya ya Madini ya mwaka 2010
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 inaelekeza wazi kuwa Madini yote nchini ni
Mali ya watanzania hivyo wanapaswa kutambua umuhimu wa rasilimali.
Wawekezaji na wachimbaji wote wa madini nchini wanapaswa
kutambua kuwa wanalo jukumu muhimu la kurejesha kwa jamii asilimia chache ya
kile wanachozalisha kwa kuunga mkono juhudi za serikali Back to the
Community) katika kuboresha miundombinu, sekta ya elimu, afya N.K
Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko
amesisitiza hayo Leo 23 Februari 2018 wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji
cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi wakati wa mkutano wa hadhara
uliofanyika katika eneo la mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe Mkoani
Rukwa Magharibi mwa Tanzania.
Mradi huo unaosimamiwa na kampuni ya Edenville Tanzania Ltd kwa
ubia na kampuni ya Edenville Energy of Uk na Upendo Group (Kampuni ya kizawa)
ilianza shughuli za majaribio ya uchimbaji na uoshaji mwezi wa kumi mwaka Jana
2017 na mkaa wa kwanza kuuzwa kwa majaribio ni mwezi Novemba mwaka 2017.
"Nataka niwajulishe tu watanzania wenzangu Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli aliniteua kusimamia Wizara
ya Madini nikimsaidia Waziri wetu Mhe Anjelina Kairuki ili kuboresha sekta hii
ya Madini hatimaye kuwanufaisha watanzania kuliko ilivyokuwa awali ambapo
Madini yalikuwa yanachimbwa nchini lakini faida inaenda nchi zingine"
Alisema Mhe Biteko na Kuongeza kuwa
Wawekezaji hao wanapaswa kutoa ajira zisizo za utaalamu kwa
wananchi wanaozunguka migodi yao sambamba na watanzania wote huku akiwaagiza
kuwaajiri wataalamu wa Madini wa ndani ya nchi kwa kazi ambazo wanaweza
kuzifanya sio kuajiri wageni.
Aidha, aliwasisitiza wananchi hao pindi wanapopata ajira zao
katika migodi mbalimbali wanapaswa kuwa waaminifu ili kuwavutia wawekezaji hao
jambo litakalopelekea wawekezaji kuwa na imani na watanzania na hatimaye
kuongeza chachu ya ajira nyingi zaidi.
Sambamba na hayo amekemea baadhi ya wafanyakazi katika migodi
mbalimbali ambao wameaminiwa na kupatiwa ajira lakini wanageuza muda wa kazi
kuwa muda wa starehe kwa kunywa pombe na utoro kazini.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko yupo katika ziara
ya kikazi ya siku mbili Mkoani Rukwa kutembelea na kukagua uchimbaji wa Madini.