Akizugumza na vyombo vya habari mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya ZFA Hussein Ali Ahmada ameeleza sababu ya kubadilisha ratiba za ligi kuu ya Zanzibar na mashindano mengine ni kutokana na uchumi wa vilabu vya Zanzibar kuwa chini hivyo changamoto ya usafiri kutoka kwenye kituo cha Unguja hadi Pemba kwa usafiri wa meli na wao ZFA hutumia meli moja tuu ya Mapinduzi ambayo wamepata punguzo la bei ya meli za tiketi na kambi za timu hizo.
Kwa upande mwengine Hussein Ali amesema sababu ya kubadilisha ratiba ya mashindano ya ZFA ni kuendana na kalenda yao ambayo itaendana na matakwa ya CAF na FIFA ili kuhakikisha itakapofika mwezi wa tano ligi kuu ya Zanzibar na mashindano yote ya ZFA tayari imeshamaliza.
Aidha amesema wao ZFA wanatarajia mwezi wa kwanza kuhakikisha dirisha dogo la usajili linafunguliwa huku michuano ya Kombe la Mapinduzi ikiendelea na wao ZFA wanaendelea na dirisha dogo la usajili ili kuwapa nafasi vilabu kusajili ili kukamilisha mzunguko wa mwisho wa Ligi kuu ya Zanzibar.
Pia ameitaja michezo ambayo imebadilishwa kwenye ratiba ni ule baina ya Gulioni na Muembeladu wa daraja la pili Taifa ambao ulikuwa uchezwe Maungani ila kwa sasa utachezwa uwanja wa Amani Jumamosi,michezo mingine ile ya Ligi kuu ya Zanzibar mzunguko wa 15 ulikuwa uchezwe Jumamosi ila michezo hiyo kwa sasa itachezwa Jumapili baina ya Polisi dhidi ya Hardrock uwanja wa Amani saa nane mchana, uwanja wa Ngome na KMKM dhidi ya Mbuyuni na Jamuhuri dhidi ya Mlandege utachezwa Amani majira ya saa Kumi za jioni michezo hiyo itachezwa Jumapili .
Katika hatua nyengine kamati hiyo ya mashindano ya ZFA imemfungia msimu mzima mwamuzi msaidizi Mohamedi Khamisi kwa kosa la kuhujumu michezo mbali mbali ya mashindano mbali mbali.
‘’Mwamuzi huyu tumemfungia lakini tunamruhusu kuendelea kubaki darasani kujifunza ila ameshindwa kutafsiri sheria ya kuotea baina ya mchezo wa Polisi na kizimbani wa ligi kuu ya Zanzibar’’ Alisema Hussein Ali Ahmada.