Baadhi ya watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Pemba,wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi inayomaliza muda wake , Abdulghani Himid Msoma , wakati wa kuagana nao kutoka na bodi hiyo kumaliza muda wake.
Na. Bakari Mussa -Pemba.
Uongozi wa mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar ,
umepongezwa kwa juhudi zake kubwa inazozichukuwa katika kutowa huduma bora kwa
wageni wanaoingia nchini hali ambayo
imeongeza mapato makubwa kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Akizungumza na Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo, Katika Kiwanja
cha ndege cha Karume Pemba, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka hiyo,
Abdughani Himid Msoma , wakati wa
kuagana na Wafanyakazi hao kufuatia kumaliza muda kwa Bodi hiyo , alisema mamlaka
ili kumbana na changamoto mbali mbali ikiwemo kuibadilisha kutoka Idara ya
Anga
hadi Mamlaka na hivyo watendaji wake walionesha Uzalendo wa hali ya juu na
kufanyakazi kwa uadilifu jambo ambalo mapato yatokanayo na Viwanja vya ndege
yameongezeka kwa asilimia kubwa.
Alieleza Bodi ya
mamlaka ya Viwanja vya ndege , ilipata mashirikiano makubwa kutoka kwa
watendaji wa Viwanja vya Ndege Unguja na Pemba, na hivyo kuiwezesha kufanyakazi
kwa weledi na ufanisi ulio mkubwa jambo ambalo limepelekea mapato kuongezeka
tafauti na kabla yakuwepo kwa mamlaka hiyo.
Msoma, aliwataka Wafanyakazi na Uongozi wa Mamlaka hiyo
kuzidisha ushirikiano , bidii na uaminifu katika kazi zao kwa kusimamia
mapato ili waweze kuisaidia Serikali
katika kukusanya mapato makubwa yatakayo iwezesha kumudu kufanya shunghuli
mbali mbali za Maendeleo.
“Wafanyakazi wa Mamlaka hii tambueni kuwa mafanikio makubwa yamekuja kutokana na ushirikiano
mkubwa muliokuwa nao baina yenu na Bodi na wafanyakazi na watendaji wenu wakuu
, hivyo naomba ushirikiano huu uendelee kwani Serikali inahitaji mapato zaidi
kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi na kuviboresha zaidi Viwanja vyenu ili
viweze kutowa huduma mzuri kwa wageni,”alisema.
Alifahamisha katika Uongozi wake wa kuiongoza Bodi hiyo kwa
muda wa miaka sita , alipata mafanikio makubwa na hivyo kuwataka wafanyakazi
hao kuwa tayari kupokea mabadiliko yatakayokuja ya Bodi mpya baada ya kuteuliwa
kwake sambamba na kuipa mashirikiano makubwa ili iweze kuleta maendeleo zaidi.
Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi hiyo inayomaliza muda wake,
Bihindi Nassor Khatib, aliwataka
watendajiwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar kuendelea kutowa huduma mzuri
kwa Wageni kwani kila mmoja ataweza kuvutika na namna anavyopata huduma na hivyo wataweza
kuongeza mapato.
Aidha, aliiomba mamlaka husika kuangalia uwezekano wa
kuongeza asawa wa ajira na hata uteuzi wa wajumbe wa Bodi kwani inaonekana
ajira kwa jinsia ya kike na uteuzi ni ndogo akitolea mfano katika Bodi hiyo
Mwanamke ni yeye peke yake.
“Tukiangalia hapa jinsia ya kike ni ndogo kwenye ajira za
Wafanyakazi wa Mamlaka hii, hata kwatika Uteuzi mjumbe ni mimi peke yangu
naomba wakati mwengine lizingatiwe hilo, “ alisema Mjumbe huyo.
Nae , Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar,
Captein, Said Iddi Ndumbogani, kwa niaba
ya Uongozi wa Mamlaka hiyo aliipongeza Bodi hiyo inayomaliza muda wake kwa
kutekeleza majukumu yao ipasavyo jambo imeipatia mafanikio makubwa mamlaka
kutokana na busara na maelekezo yao yanalioendana na ufanisi wa kazi za kila
siku.
Aliwataka Wafanyakazi kuendelea kufanyakazi kwa bidii
sambamba na kufanyakazi kwa kufuata maelekezo yaliokuwa yanatolewa na Bodi hiyo
, ili waweze kujiletea maendeleo zaidi .
“Bodi ilikuwa ikituelekeza sana katika mambo mbali mbali ya
ufanisi wa majukumu yetu ya kazi za kila siku, hivyo nawaomba wafanyakazi
wenzangu tuzidi kushikamana kufanyakazi kwa weledi na Uaminifu kama tulivyokuwa
tukisimamiwa na Bodi hii, inayomaliza muda wake,” alieleza.
Nae, Mwanasheria wa Bodi hiyo , Awadhi Ali Said, aliwasihi
Wafanyakazi kuendelea kufanyakazi zao kwa bidi na maarifa yatakayopelekea
kufikia malengo yaliowekwa na Serikali juu ya kuwepo kwa Viwanja vya ndege vya
kisasa Zanzibar kwa ajili ya kukuza Utalii na kuongeza mapato ya Taifa.
Alisema ili kufikia malengo makubwa na ya kweli ni vyema kwa
watendaji hao kukaa na kujipima kutokana na huduma wanazozitowa ambazo
zitawavutia wageni wanaoingia , ikiwemo Watalii.
Kwa upande wake , Makamo mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya ndege inayomaliza muda
wake , Hamad Bakar Mshindo, aliwataka wafanyakazi kufanyakazi zao kwa kufuata
misingi ya kanuni za utumishi wa Serikalini jambo ambalo wataweza kumtumikia
mwajiri wao ipasavyo na wao kuweza kupata haki zao bila ya matatizo.
Aliwasihi wafanyakazi hao kuzidisha bidii katika kazi na
kuipa mashirikiano ya kiutendaji Bodi mpya itakayokuja kwa misingi ya kuleta
mafanikio katika Mamlaka hiyo , kama vile walivyokuwa wakiipa mashirikiano Bodi
inayoondoka.