TAARIFA
YA MATOKEO YA MITIHANI YA TAIFA YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SITA NA
DARASA LA NNE YA MWAKA 2017, JUMATATU TAREHE 29 JANUARI 2018.
1.0 UTANGULIZI
Ndugu
Wazazi, Wanafunzi, Walimu na Wananchi wote na waandishi wa Habari.
Ndugu Waandishi wa Habari, leo Jumatatu tarehe 29 Januari 2018,
nimewaita ili kuzungumzia kuhusu matokeo ya mitihani ya Taifa ya Darasa
la Nne, Darasa la Sita na Kidato cha Pili ya mwaka 2017 ambayo
ilifanyika kuanzia tarehe 20/11/2017 na kumalizika tarehe 06/12/2017.
Mitihani hiyo ilishirikisha skuli zote za Serikali na za Binafsi.
Matokeo ya mitihani hiyo ndio kigezo kinachotumika rasmi kitaifa kwa
wanafunzi wa Zanzibar katika ngazi hizo na kila skuli iliyofanya
mitihani huu inapaswa kuyatumia matokeo hayo. Kwa mitihani ya Kiadto cha
Pili mwaka 2017, kulikuwa na makundi mawili ya watahiniwa wa Kidato cha
Pili waliomaliza Elimu ngazi ya Msingi mwaka 2015, Kundi la kwanza
walimalizia elimu ya msingi Darasa la Saba (F.II - 7) na kundi la pili
walimaliza elimu ya msingi Darasa la Sita (F.II - 6). Wote hawa
waliingia Kidato cha 1 pamoja mwaka 2016 na kufanya Mtihani wa pamoja wa
Kidato cha Pili mwaka 2017.
Ndugu Wazazi, Walimu, Wanafunzi na Wananchi,
Wanafunzi
waliofanya Mtihani wa Kidato cha Pili (6) mwaka 2017 ni wanafunzi
walioingia Darasa la Kwanza mwaka 2010 na kumaliza elimu ya msingi ya
miaka 6 mwaka 2015 kwa mujibu wa Sera ya Elimu ya mwaka 2006.
Kwa
mujibu wa Sera ya Elimu ya mwaka 2006, elimu ya lazima kwa wanafunzi wa
Zanzibar ni miaka 12, kwa utaratibu wa miaka 2 ya elimu ya maandalizi,
miaka 6 ya msingi na miaka 4 ya elimu ya sekondari hadi Kidato cha Nne.
Hivyo, kwa watahiniwa wa Kidato cha Pili wa mwaka 2017, waliomaliza
Elimu ya msingi (kwa miaka sita) na ambao wamepata alama za jumla za
wastani chini ya Daraja D, watarudia tena masomo ya kidato cha Pili
katika skuli zao na watafanya tena Mtihani wa kidato cha Pili mwaka
2018. Watahiniwa hao waliopata alama za daraja la chini ya D waliosoma
Msingi kwa muda wa miaka 6 ni 5,789. Kufanya hivyo ni utekelezaji wa
Sera ya Elimu inayoelekeza wanafunzi wapate elimu ya miaka 12 hadi
Kidato cha Nne. Napenda kusisitiza kuwa watakaorudia ni wale tu
waliofanya mtihani na kupata alama wastani wa chini wa D na wala sio
waliokuwa hawakufanya mtihani kwa sababu ambazo hazikutambulika.
Wanafunzi
waliofanya mtihani wa Kidato cha Pili 2017 na kusoma elimu ya msingi
kwa miaka 7 ambao wamepata wastani wa alama chini ya D hawatorudia
masomo yao kwani wao walifuata mfumo tofauti na huu.
Kwa
taarifa hii Walimu Wakuu wanatakiwa kutompokea mwananafunzi anaerudia
masomo ambae hayumo kwenye utaratibu ulioelezwa. Pia, napenda
kuwajulisha wanafunzi, walimu na wazazi kuwa haki ya kupata elimu hadi
kidato cha Nne kwa wanafunzi wa Skuli za sekondari haimaanishi kuwa
mwanafunzi ataendelea na masomo bila ya kupimwa na kufaulu. Mwanafunzi
atakaepata wastani wa chini atarudia kabla ya kuendelea na masomo yake.
Ndugu Wananchi, Walimu, Wanafunzi na Waandishi wa Habari,
2. KIDATO CHA PILI
2.1. UANDIKISHAJI
Jumla
ya watahiniwa 49,515 kutoka Kidato cha Pili (6) na Kidato cha Pili (7)
wamesajiliwa kufanya mtihani wa kuingia Kidato cha Pili mwaka 2017 ambao
ni sawa na ongezeko la asilimia 45.42 ikilinganishwa na watahiniwa
27,017 sawa asilimia 52.5 waliofanya mtihani mwaka 2016.
Katika
uandikishaji huo, watahiniwa wa kike ni 27,239 sawa na asilimia 55.01
na wa kiume ni 22,276 sawa na asilimia 44.99 waliandikishwa. Watahiniwa
wa kidato cha Pili (6) ni 22,207 wakiwemo wanawake 12,930 na wanaume
9,277 na kwa watahiniwa wa Kidato cha Pili (7) ni 27,308 wakiwemo
wanawake 14,309 na wanaume 12,999.
2.2 UFANYAJI WA MTIHANI
Jumla
ya watahiniwa 46,580 walifanya mtihani wa Kidato cha Pili sawa na
asilimia 94.07 ya walioandikishwa wakiwemo wanawake 26,061 sawa na
asilimia 55.95 na wanaume 20,519 sawa na asilimia 44.05.
Kati
ya watahiniwa hao, watahiniwa 20,887 ni wa Kidato cha Pili (6) wakiwemo
wanawake 12,368 na wanaume 8,519 na watahiniwa 25,693 wakiwemo
wanawake 13,693 na wanaume 12,000 ni wa Kidato cha Pili (7). Wanafunzi
2,935 hawakufanya mitihani yao.
2.3 MATOKEO YA MTIHANI
Jumla
ya watahiniwa 34,458 sawa na asilimia 73.98 ya watahiniwa wote
wamefaulu, kati yao wanawake ni 20,793 sawa na asilimia 60.34 na wanaume
ni 13,665 sawa na asilimia 39.66. Ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.88
ukilinganisha na watahiniwa 17,581 sawa na asilimia 70.1 kwa mwaka 2016.
Watahiniwa 12,122 hawakufaulu wakiwemo 5,789 wa Kidato cha Pili (6) na
6,333 wa Kidato cha Pili (7) sawa na asilimia 26.02.
Kwa
Kidato cha Pili (6) watahiniwa waliofaulu ni 15,098 sawa na asilimia
72.28 wakiwemo wanawake 9,650 sawa na asilimia 46.20 na wanaume 5,448
sawa na asilimia 26.08. Kwa upande wa Kidato cha pili (7) watahiniwa
waliofaulu ni 19,360 sawa na asilimia 75.35 wakiwemo wanawake 11,143
sawa na asilimia 43.37 na wanaume 8,217 sawa na asilimia 31.98. Hivyo
asilimia ya ufaulu wa watahiniwa wa kike ni mkubwa kuliko wa kiume. Pia,
asilimia ya ufaulu wa watahiniwa wa Kidato cha Pili (7) ni mkubwa kwa
asilimia 3.07 ukilinganisha na watahiniwa wa Kidato cha Pili (6).
3. DARASA LA SITA
3.1 UANDIKISHAJI
Jumla
ya watahiniwa 34,444 waliandikishwa kwa ajili ya kufanya mitihani wa
kumalizia elimu ya msingi darasa la Sita mwaka 2017 wakiwemo Wanawake
18,064 sawa na asilimia 52.44 na Wanaume 16,380 sawa na asilimia 47.56.
Hii ni ongezeko la asilimia 3.6 ukilinganisha na watahiniwa wa mwaka
2016 ambao walikuwa ni 33,250.
3.2 UFANYAJI WA MITIHANI
Jumla
ya watahiniwa 32,379 sawa na asilimia 94.0 ya walioandikishwa walifanya
mtihani wa darasa la sita wakiwemo wanawake 17,421 sawa na asilimia
53.8 na wanaume 14,958 sawa na asilimia 46.20.
3.3 MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SITA 2017
Jumla
ya watahiniwa 31,145 sawa na asilimia 96.19 wamefaulu kuingia Kidato
cha Kwanza 2018, kati yao Vipawa ni 138 sawa na asilimia 0.44. Michepuo
ni 1,387 sawa na asilimia 4.45 na wale wanaoendelea na masomo yao
katika Sekondari za kawaida ni 29,620 sawa na asilimia 95.11. Ufaulu huu
ni sawa na ongezeko la asilimia 0.99 ukilinganisha na watahiniwa 29,413
sawa na asilimia 95.2 wa mwaka 2016. Aidha watahiniwa 1,234 hawakufaulu
mtihani sawa na asilimia 3.81. Idadi ya watahiniwa waliofaulu vipawa
imeongezeka kutoka 71 wa mwaka 2016 hadi 138 kwa mwaka 2017. Pia,
idadi ya watahiniwa waliofaulu kuingia michepuo imeongozeka kutoka 889
mwaka 2016 hadi kufikia 1,387 mwaka 2017.
4. DARASA LA NNE
4.1 UANDIKISHAJI
Jumla
ya watahiniwa 40,206 waliandikishwa kwa ajili ya kufanya mitihani. Kati
yao wa kike ni 20,260 sawa na asilimia 50.39 na Wa kiume 19,946 sawa na
asilimia 49.61. Idadi ya watahiniwa imeongezeka kutoka 38,681 mwaka
2016 hadi kufikia 40,206 kwa mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia
3.9.
4.2 UFANYAJI WA MITIHANI
Jumla ya watahiniwa 37,139 walifanya mtihani wa Darasa la Nne mwaka
2017 sawa na asilimia 92.37 ya walioandikishwa. Kati yao watahiniwa wa
kike ni 19,068 sawa na asilimia 51.34 na wa kiume 18,071 sawa na
asilimia 48.66. Wanafunzi 3,067 hawakufanya mtihani sawa na asilimia
7.63 ambao ni pungufu ukilinganisha na watahiniwa 4,015 sawa na asilimia
10.4 kwa mwaka 2016.
4.3 MATOKEO
Jumla
ya watahiniwa 26,448 sawa na asilimia 71.21 walifaulu mtihani wao kati
yao watahiniwa wa kike 14,764 sawa na asilimia 55.82 na wa kiume 11,684
sawa na asilimia 44.18. Ufaulu huu ni ongezeko la asilimia 18.11
ukilinganisha na watahiniwa 18,423 sawa na asilimia 53.1 waliofaulu
mwaka 2016. Watahiniwa 10,691 sawa na asilimia 28.79 hawakufaulu
mtihani. Idadi hii ni ndogo ukilinganisha na watahiniwa 16,258 sawa na
asilimia 46.88 kwa mwaka.
5. WANAFUNZI KUMI BORA
KIDATO CHA PILI
Katika mtihani wa Kidato cha Pili mwaka 2017, wanafunzi bora kitaifa ni kama ifuatavyo:
KIDATO CHA PILI (6)
NO JINA SKULI NAM. YA MTIHANI
1. MARYAM AMOUR JUMA FIDEL CASTRO ZS.189/024
2. MUNDHIR SALIM ALI FIDEL CASTRO ZS. 189/051
3. AHMED KHALFAN ABDALLAH FIDEL CASTRO ZS. 189/043
4. SEIF KHAMIS NASSOR FIDEL CASTRO ZS. 189/055
5. BASWIRA ALI JUMA FEZA ZS.232/006
6. LAYTH NAQUEEB JAWAD FEZA ZS.232/032
7. ANWAR HAIDAR HEMED FIDEL CASTRO ZS. 189/044
8. MUSTAFA KHAMIS SHAABAN LUMUMBA ZS.19/048
9. NADHIFA RAMADHAN SOUD FIDEL CASTRO ZS. 189/028
10. JAMILA IBRAHIIM MOH’D FIDEL CASTRO ZS. 189/020
KIDATO CHA PILI (7)
NO JINA SKULI NAM. YA MTIHANI
1. RAUDHAT ABDALLA MSELLEM FIDEL CASTRO ZS.189/028
2. FIDAUS SALUM SEIF MAHAD ISTIQAMA ZS.247/005
3. RAYA ISSA RAMADHAN LUMUMBA ZS. 019/028
4. FARHAT FEREJ ABDULHABIB LAUREATE ZS. 233/012
5. MARCO ANDREA MASABUDA MIKINDANI ZS. 045/038
6. LUTTFIYYA ABDALLAH SALIM MAHAD ISTIQAMA ZS. 247/013
7. NAJAT WALID KASSIM LAUREATE INT. ZS.233/036
8. SUMAYYA AHMAD YAKOUB LAUREATE INT. ZS.233/059
9. ABDUL-KADIR SALIM HAMAD FIDEL CASTRO ZS.189/039
10. SEIF SELEIMAN SEIF SUNNI MADRESSA ZS. 213/074
DARASA LA SITA
Katika mwaka wa masomo wa 2017 wanafunzi bora kwa mtihani wa darasa la sita ni hawa wafuatao:
NO JINA SKULI NAM. YA MTIHANI
1. MUNIRA RASHID MOH’D KIJITOUPELE ‘A’ ZP.060/125
2. HAITHAM TAHIR MUSSA LAUREATE INT. (P) ZP.384/003
3. HAITHAM OMAR ABDALLA MICHAKAINI ‘B’ ZP.217/029
4. HAMID TAHIR MUSSA LAUREATE INT. (P) ZP.384/013
5. KHALFAN MASSOUD SALUM TUMBE ZP.195/182
6. MIKIDADI JUMA ALI MITIULAYA ZP.180/175
7. AYOUB RASHID AHMAD KIZIMBANI PEMBA ZP.181/103
8. HUMOUD MASSOUD FADHIL LAUREATE INT. (P) ZP.384/014
9. ABDUL-MUSAWIR HIJA HAJI MTONI MSINGI ZP.054/149
10. KHADIJA KHAMIS SHEHA MTOTEPO ‘B’ ZP.035/086
DARASA LA NNE
Katika mwaka wa masomo wa 2017 wanafunzi kumi bora ni kama ifuatavyo.
NO JINA SKULI NAM. YA MTIHANI
1. ARIF SULEIMAN ALLEY FRANCIS MARIA ZP.372/065
2. UMMUKULTHUM JUMA ALI MITIULAYA ZP.180/096
3. SHAIB HAMAD SHAIB KONDE ISTIQAMA ZP.285/043
4. HAJRA NASSOR KHALAIF GLORIOUS ACADEMY ZP.342/040
5. SHAAME NYANGE ALI P/MCHANGANI ZP.056/059
6. ENAAN JOHAN VANDENABEELE FEZA ZP.304/023
7. FADHIL HUSSEIN MWAIBU MAKADARA ZP.020/053
8. FATMA SHAIB ALI KIZIMBANI PEMBA ZP.181/020
9. AISHA RAHIM ALI MADUNGU MSINGI ZP.224/006
10. INTISAAR OMAR HAMAD JADIDA ZP.182/070
5.1 SKULI ZENYE WASTANI MKUBWA KITAIFA
Zifuatazo ni skuli zenye wastani mkubwa kitaifa katika Mtihani wa kidato cha Pili.
KIDATO CHA PILI (6)
NO SKULI NA WILAYA
1. FIDELCASTRO – CHAKE- CHAKE PEMBA
2. LUMUMBA – MJINI UNGUJA
3. MADUNGU ‘B’ – CHAKE- CHAKE PEMBA
4. TUMEKUJA – MJINI UNGUJA
5. BENBELLA – MJINI UNGUJA
6. MIKUNGUNI – MJINI UNGUJA
7. KIEMBE SAMAKI ‘A’ MCHEPUO – MAGHARIBI “B”
8. MAHAD ISTIQAMA – KATI UNGUJA
9. ZANZIBAR COMMERCIAL – MAGHARIBI “B”
10. CHASASA ‘B’ – WETE PEMBA
KIDATO CHA PILI (7)
NO SKULI
1. FIDELCASTRO - CHAKE CHAKE, PEMBA
2. LUMUMBA – MJINI UNGUJA
3. S.O.S HERMANN – MAGHARIBI “B” UNGUJA
4. CHASASA ‘B’ – WETE,PEMBA
5. LAUREATE INTERNATIONAL – MAGHARIBI “B” UNGUJA
6. MAHAD ISTIQAMA – KATI UNGUJA
7. BENBELLA – MJINI UNGUJA
8. SUNNI MADRESSA – MJINI UNGUJA
9. FRANCIS MARIA – MAGHARIBI “B” UNGUJA
10. J.K.U MTONI – MJINI UNGUJA
DARASA LA SITA MWAKA 2017
NO SKULI
1. S.O.S HERMANN – MAGHARIBI “B” UNGUJA
2. GLORIUS ACADEMY – MJINI UNGUJA
3. ENGLISH SPEAKING – MJINI, UNGUJA
4. MAHAD ISTIQAMA – KATI, UNGUJA
5. ALI KHAMIS CAMP – CHAKE CHAKE PEMBA
6. LAUREATE INTERNATIONAL – MAGHARIBI “B” UNGUJA
7. RAUDHA ACADEMY – MAGHARIBI “B” UNGUJA
8. TRIFONIA ACADEMY – MAGHARIBI “B” UNGUJA
9. DONGE MSINGI – KASKAZINI “B” UNGUJA
10. HIGH VIEW INTERNATIONAL – MAGHARIBI “B” UNGUJA
DARASA LA NNE
NO SKULI
1. GLORIOUS ACADEMY – MJINI UNGUJA
2. ALI KHAMIS CAMP – CHAKE CHAKE, PEMBA
3. FRANCIS MARIA – MAGHARIBI “B” UNGUJA
4. LAUREATE INTERNATIONAL- MAGHARIBI “B” UNGUJA
5. MEMON ACADEMY - MJINI , UNGUJA
6. BILAL ISLAMIC – MJINI, UNGUJA
7. S.O.S HERMANN – MAGHARIBI “B” UNGUJA
8. ALHARAMAYN INTENATIONAL – MAGHARIBI “B” UNGUJA
9. KONDE ISTIQAMA – MICHEWENI, PEMBA
10. HIGH VIEW INTERNATIONAL – MAGHARIBI “B” UNGUJA
5.2 SKULI ZENYE WASTANI MDOGO KITAIFA
KIDATO CHA PILI (6)
NO SKULI WILAYA
1. KIBENI Kaskazini “A” Unguja
2. KIZIMKAZI Kusini Unguja
3. MUYUNI Kusini Unguja
4. UNGUJA UKUU Kusini Unguja
5. UROA Kusini Unguja
6. KILINDI Kusini Pemba
7. MBUZINI UNGUJA Magharibi “ A” Unguja
8. MLIMANI MATEMWE Kaskazini “A” Unguja
9. JAMBIANI Kusini Unguja
10. MWENGE Magharibi “ A” Unguja
KIDATO CHA PILI (7)
NO SKULI WASTANI
1. KISIWA PANZA Mkoani Pemba
2. UNGUJA UKUU Kati, Unguja
3. MIZINGANI Mkoani, Pemba
4. KOMBENI Magharibi “B” Unguja
5. KENGEJA Mkoani, Pemba
6. GAMBA Kaskazini “A” Unguja
7. KIBENI Kaskazi “A” Unguja
8. KUSINI Kusini, Unguja
9. JAMBIANI Kusini, Unguja
10. UROA Kusini, Unguja
DARASA LA SITA
NO SKULI WILAYA
1. KILOMBERO Kaskazini “B” Unguja
2. MTANGANI Mkoani, Pemba
3. KIANGA Magharibi “A” Unguja
4. HAROUN PEMBA Micheweni
5. PETE Kati, Unguja
6. SEBLENI Mjini
7. MKWAJUNI Kaskazini A”
8. UZI Kati, Unguja
9. TUMBATU Kaskazini A, Unguja
10. BWEFUM Magharibi “B” Unguja
DARASA LA NNE
NO SKULI WILAYA
1. CHAMBANI Mkoani, Pemba
2. MWAMBE Mkoani, Pemba
3. MBUYUTENDE Kaskazini “A” Unguja
4. KANDWI Kaskazini “A” Unguja
5. KILOMBERO Kaskazini “B” Unguja
6. KARUME PEMBA Micheweni, Pemba
7. UONDWE Wete, Pemba
8. NUNGWI Kaskazini “A” Unguja
9. TUMBATU Kaskazini “A” Unguja
10. MTANGANI Mkoani, Pemba
6. WATAHINIWA WASIOFANYA MITIHANI
Jumla
ya watahiniwa 2,935 wa kidato cha Pili (1,320 wa Kidato cha Pili (6) na
1,615 wa Kidato cha pili (7). Pia, watahiniwa 2,066 wa Darasa la Sita
na 3,068 wa Darasa la Nne hawakufanya mitihani hii. Miongoni mwa sababu
za kutofanya mitihani hii ni utoro, ugonjwa, ndoa, uhamisho na
kufariki.
KIDATO CHA PILI
SABABU UTORO UHAMISHO UGONJWA NDOA KIFO JUMLA
KIDATO CHA PILI (6) 1,305 2 11 2 1,320
KIDATO CHA PILI (7) 1,590 3 16 5 1 1,615
JUMLA 2,895 5 27 5 3 2,935
DARASA LA SITA
SABABU UTORO UHAMISHO UGONJWA NDOA KIFO JUMLA
IDADI 2,018 18 27 1 1 2,065
DARASA LA NNE
SABABU UTORO UHAMISHO UGONJWA NDOA KIFO JUMLA
IDADI 2,996 48 22 - 2 3,068
7. KESI ZA UDANGANYIFU
Kwa
mwaka 2017, hakuna kesi ya udanganyifu iliyoripotiwa kwa watahiniwa wa
Darasa la Sita na Darasa la Nne. Jumla ya watahiniwa wanane (8) wa
Kidato cha Pili walithibitika kufanya udanganyifu kwa kuwa na vipande
vya karatasi vyenye maandishi huku wakifanya mitihani yao. Kitendo
ambacho ni kinyume na kanuni za mitihani. Hivyo wanafunzi wote hawa
waliothibitika kufanya udanganyifu huo wamefutiwa matokeo yao kwa mujibu
wa kanuni ya 58(1) ya Kanuni za Baraza la mitihani la Zanzibar.
Watahiniwa hao ni kutoka Skuli za Fujoni, Mwanakwerekwe “B”, Kwa Mtipura na Chuini. Watahaniwa hao ni wenye nambari zifuatazo:-
ZS.74/39/7 ZS.34/150/7
ZS.74/33/7 ZS.34/159/7
ZS.74/13/7 ZS.12/512/7
ZS.34/126/7 ZS.30/1003/6
8. MWISHO
Kwa
niaba ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, tunawapongeza wale wote
waliofanikiwa kuendelea na masomo na tunawatakia kila la kheri katika
masomo yao. Pia, nawatakia mafanikio mema wanafunzi watakaorudia masomo
ya Kidato cha Pili, nataraji kuwa watafanya bidii katika masomo yao ili
waweze kupata matokeo mazuri katika mtihani wa marejeo. Aidha,
tunawajuilisha wazazi na walimu wakuu kwamba wanafunzi wote wa madarasa
ya Nne na Sita ambao hawakufanya mitihani husika kwa sababu zozote zile
watalazimika kurudia madarasa hayo na kufanya tena mitihani mwisho wa
mwaka 2018.
Kwa
wanafunzi wa Kidato cha Pili ambao wamemaliza Kidato cha pili (7) ambao
hawakufaulu tunawasihi wasivunjike moyo na tunawashauri Wazazi/Walezi
wawapeleke kwenye Vituo vya Kujiendeleza viliopo karibu nao.
Wanafunzi
waliofaulu kipawa na michepuo tu ndio watatangazwa kwenye ZBC – Redio.
Wanafunzi wa Kidato cha Pili matokeo yao yatapatikana katika vituo vyao
walivyofanyia mitihani au kupitia tovuti ya Wizara ambayo ni
www.moez.go.tz . pia kupitia facebook ya Wizara ‘Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Amali’
Wizara
inatoa shukrani za dhati kwa Wazazi, Walimu, na wale wote
walioshirikiana nasi katika kufanikisha kazi hii muhimu sana ya Mitihani
ya Taifa.