
Ligi ya mabingwa barani ulaya imeendelea jana kwa michezo kadhaa ya makundi, kundi E, AEK Athens imekubali kipigo cha bao 2-0 toka kwa Ajax. Nayo FC Bayern Munchen ikiifyatua Benfica kwa jumla ya mabao 5-1. Kundi F, Hoffenheim imefungwa 3-2 na Shakhtar Donetsk, huku Lyon ikiilazimisha Manchester City sare ya 2-2.
CSKA Moscow imalala kwa goli 2-1 dhidi ya Victoria Plzen, huku Real Madrid ikiitungua AC Roma 2-0 katika michezo wa kundi G.
matokeo ya kundi H, Juventus imeilaza Valencia kwa ushindi mdogo wa goli 1-0, nayo Manchester United imeifunga Young Boy goli 1-0.