Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
Na Anitha Jonas –
WHUSM, Dar es Salaam
Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) Gianni Infantino na Rais wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Afrika (CAF) Ahmad Ahmad wakiri kuelewa hali ya Zanzibar pamoja na
kuzingatia Sheria wamesema wanaona mazingira Maalum ya Zanzibar.
Kauli hiyo imetolewa
leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
mambo mbalimbali serikali iliyozungumza na Marais hao wa mashirikisho ya mpira
wa miguu kwa ngazi ya bara la Afrika na Dunia walipofika nchini hivi karibuni
kwa ajili ya kufanya mkutano wao wa kuandaa ajenda za mkutano mkuu wa dunia.
‘’Marais
hao walisema
kuondolewa kwa Zanzibar katika uanachama wa CAF kulizingatia sheria
zinazosimamia Shirikisho hilo lakini pamoja na hayo waliamua kuiachia
Zanzibar kuendelea kufaidika na fursa zote wanazopatiwa wanachama wa
CAF isipokuwa kuwaruhusu kupiga kura, pia wanasema
wataangalia zaidi ya hilo maeneo mengine namna ya kuisaidia
Zanzibar,''Dkt.Harrison Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza
katika Mkutano huo Mheshimiwa Mwakyembe alisisitiza kuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa
Kassim Majaliwa alieleza kwa ufasaha mgogoro huu wa soka kwa viongozi hao
wenyedhamana na mashirikisho hayo nao kumuelewa ambapo walisisitiza kuhitaji
serikali kuendelea kushauriana nao katika suala hilo.