Habari kamili: Askari ‘Magereza’ Kengeja anaedaiwa kumuingilia mlemavu wa akili apandishwa mahakamani - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, November 03, 2018

Habari kamili: Askari ‘Magereza’ Kengeja anaedaiwa kumuingilia mlemavu wa akili apandishwa mahakamani

HABARI KUU
HATIMAE askari wa Chuo cha Mafunzo Kengeja wilaya ya Mkoani Pemba, Sleyoum Idd Saleh miaka 30, aliedaiwa kumuingilia mlemavu wa akili, amepandishwa katika kizimba cha mahakama ya Mkoa Chakechake, kujibu tuhuma zinazomkabili.
Mtuhumiwa huyo alipandishwa mahakamani hapo, Novemba 2, mwaka huu, ambapo baada ya kutua kizimbani, wakili wa serikali na mwendesha mashtaka kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Ali Amour Makame, alimsomea shitaka lake.
Amour, alidai mahakamani hapo kuwa, katika siku isiofahamika mwezi April mwaka huu, askari huyo alimuingilia mlemavu wa akili majira saa 2:30 usiku kijijini kwao Kengeja.
Mwendesha mashitaka huyo alidai kuwa, mtuhumiwa Sleyoum alitenda kosa hilo, huku akijua kuwa, anaemuingilia ni mlemavu wa akili, ambapo kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 116 (1) cha cheria no 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.
“Sleyoum unatuhumiwa kumuingilia mlemavu wa akili mwenye miaka 25 shehia ya Kengeja, ambapo wakati unafanya hivyo ulikuwa unajua kuwa, ni mlemavu wa akili,”alidai Mwendesha mashtaka huyo mahakamani hapo.
Mara baada ya Mwendesha mashitaka huyo kumaliza kumsomea tuhuma zinazomkabili mtuhumiwa huyo, Hakimu wa mahakama ya Mkoa Chakechake Khamis Ali Simai, aliuuliza upande wa mashitaka, ikiwa una lolote.
“Ehee… upande wa mashitaka mnasemaje, ambapo Mwendesha mashitaka aliieleza mahakama hiyo kuwa, tayari upelelezi umeshakamilika na kuiomba mahakama ipange siku nyengine kwa ajili ya kusikilizwa mahashidi,”alidai.
Baada ya mtuhumiwa huyo kuomba dhamana, Hakimu Khamis aliuuliza upande wa mashitaka na kusema kuwa, kosa lake ni miongoni mwa makosa yenye dhamana, ambapo Hakimu alimapa masharti ya dhamana na kuyamudu.
“Dhamana yako iko wazi, ambapo wewe uandikishe dhamana ya shilingi milioni 1, na wadhamini wawili wenye kima kama hicho na barua za sheha na vitambulisho kama watavipata,”alisema Hakim Khamis.
Ambapo mtuhumiwa huyo, amesalimika kwenda chuo cha mafunzo baada ya kuyatimiza masharti hayo, na shauri lake limepangwa kusikilizwa tena Novemba 15 mwaka huu.
Huku hakimu Khamis, akiutaka upande wa mashitaka kuwaita mashahidi na kufika siku hiyo, ili kuja kutoa ushahidi mbele ya mtuhumiwa huyo.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI