Waokoaji wa zao la karafuu 191 waanguka, wanne wapoteza maisha…… - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, May 09, 2018

Waokoaji wa zao la karafuu 191 waanguka, wanne wapoteza maisha……

HABARI KUU


JUMLA ya waokoaji wa zao la karafuu 191, wameripotiwa kuanguka mikarafuu kwa Unguja na Pemba, huku wanne (4) wakifariki dunia katika msimu huu unaomalizia wa mwaka 2017/2018,.
Akizungumza katika Mkutano wa tahmini wa utekelezaji wa kazi za Wizara kwa msimu huu, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi katika shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Kassim Maalim Suleiman alisema, idadi ya walioanguka mikarafuu imeongezeka ukilinganisha na msimu uliopita.
Alisema kuwa, msimu wa mwaka 2016/2017walianguka mikarafuu wananchi 63, ambapo msimu uliomalizia wa mwaka 2017/2018 ni wananchi 191 walianguka mikarafuu.
“Wananchi hao walioanguka kwenye mkarafuu sehemu mbali mbali za Unguja na Pemba, tayari wameshakatiwa bima yao ya Afya ili kuweza kuwasaidia”, alisema Mwenyekiti huyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Karafuu, Ali Suleiman Mussa alisema ZSTC, kwa kushirikiana na Shirika la Bima la Zanzibar ‘ZIC’ limehakikisha wanapata matibabu na kwa sasa kinachofanyika ni kuhakikisha wananchi hao wanalipwa fidia zao.
“Idadi ya watu waliongaku mikarafuu ni kubwa zaidi kwa msimu kuliko tulivyotarajia na tayari sasa wameshafanyiwa utaratibu wa malipo,” alieleza Mkurugenzi huyo.
Mapema akifungua Mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, alisema kuwepo kwa ushirikiano na uzalendo kwa wakulima hao katika kuhakikisha wanauza zao hilo serikali, limeweza kuleta mafanikio makubwa .
“Iwapo juhudi hizi zitaendeleza, Serikali itaingiza pato la Taifa, na kuwanufaisha wakulima na wananchi kwa ujumla katika nyanja za kiuchumi,” alisma Mkuu huyo.
Aidha aliliomba shirika la ZSCT kuhakikisha zao hilo linalindwa, ili lisiweze kutoka kwa njia yoyote, sambamba na kusimmia upatikanaji wa zao hilo na kuhakikisha linauzwa kwenye shirika hilo.
Akichangia mada katika mkutano huo, Salum Khamis kutoka shehia ya Shungi aliiomba Wizara ya kilimo kuwasaidia kwa kuwapa miche ya mikarafuu mara mbili kwa mwaka, ili kuweza kupata mikarafuu ambayo itawatosheleza wakulima.
Nae Issa Khamis Yussuf mkaazi wa shehia ya Mgelema aliiomba serikali, kufikiria upya suala la ukodishwaji wa mashamba ya mikarafuu, ili kuweza kuwasaidia wakulima.
“Mtu anafyeka shamba na kupanda mkarafuu zaidi ya miaka 20, lakini kwa siku hizi anaambiwa ni la serikali na wanalikodisha, jmbo ambalo linatukosesha haki zetu maana hicho tulichoambiwa tutapewa ni kidogo ukilinganisha na kazi ngumu tulizozifanya”, alisema mkulima huyo.
Mkutano huo ulioandaliwa kwa wakulima wa zao la karafuu Wilaya ya Chake Chake ulifanyika katika Ukumbi wa Makonyo.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI