Kocha mkuu wa Mtibw Sugar Zubery Katwila amesema ushindi waliopata dhidi ya Azam kwenye mchezo wa Azam Sports Federation Cup na kuifunga 3-0 Singida United kwenye mchezo wa ligi itakuwa chachu kwenye mchezo wao dhidi ya Simba uwanja wa Jamhuri.
“Matokeo ya ushindi dhidi ya Singida United yanaweza kuwa chachu ya ushindi kwenye mchezo wa Simba kwa sababu kushinda kunaleta hamasa na morali katika timu kuelekea mchezo unaofuata”-Zubery Katwila.
“Tulitambua kama tutakuna na Simba ambayo kweli kwa sasa inafanya vizuri kwa hiyo ni vijana wenyewe kupunguza makosa ambayo yanaweza kutugharimu.”
“Wachezaji wote wako vizuri kila mmoja ana ari ya kucheza na ushindi kwa sababu tulianza vibaya raundi ya pili yakasemwa maneno mengi lakini hakukuwa na kitu kingine cha ajabu tulikosa matokeo lakini tumetulia kila kitu kinaenda sawa.”
Mtibwa Sugar itawakosa wachezaji wake muhimu kutokana na majeraha na kutumikia adhabu ya kadi.
“Kuna wachezaji ambao naweza kuwakosa kwenye mchezo dhidi ya Simba, Issa Rashidi, Salum Kanoni lakini Mohamed Issa ‘Banka’ anaweza akacheza au asicheze. Kelvin Sabato ‘Kiduku’ anakadi tatu za njano kwa hiyo na yeye tutamkosa lakini wengine wako vizuri.”