Wanahabari
Hellena Mwango, Careen , Kulwa Mwaibale na mke wa Patrick Mwillongo
wakiwa wamekaa nje ya jengo la Hospitali ya Mkoa Temeke wakitafakari
namna ya kumsaidia Mwillongo walipofika kumjulia hali leo hii asubuhi.
Na Mwandishi Wetu
Ndugu wanahabari mwenzetu Patrick Mwillongo yupo hoi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ambako amelazwa kwa matibabu.
Mwillongo anasumbuliwa na ugonjwa wa kujaa maji kwenye mapafu ambao umesababisha hashindwe kujimudu kufanya jambo lolote.
Kwa umoja wetu na tabia tuliojijengea kama wanahabari tujitokeze kumsaidia mwenzetu ambaye anapita katika kipindi kigumu.
Mwillongo ni Mwandishi wa Habari wa kujitegemea
na
anafanya shughuli zake wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na awali alikuwa
akiandikia magazeti mbalimbali likiwemo Jambo Leo na yale yanayomilikiwa
na Kampuni ya New Habari.
Kwa atakayegusa kumsaidia anaweza kutoa mchango wake kupitia namba MPESA-0754362990, Tigo Pesa ni 0712727062.