HABARI KUU
Manchester United wana tatizo juu ya Paul Pogba. Ni mchezaji
muhimu ambaye bila uwepo wake ni shida, lakini pia anayefanya maisha
kuwa magumu kwa kwa kikosi cha Jose Mourinho pindi anapopewa majukumu
ambayo hana uwezo nayo.
Na kuthibitisha hilo katika mchezo dhidi ya Tottenham Hotspur katika
dimba la Wembley juzi Jumatano, Pogba alionyesha kiwango kidhaifu zaidi
tangu ajiunge na United, na baada ya dakika 62 alitolewa nje na kocha
wake Jose Mourinho. Timu yake ikiwa nyuma kwa magoli 2-0 na bado wakiwa
wanapigiwa mpira mwingi na Spurs, ambao wachezaji wake 11 walikuwa na
majukumu ambayo waliyamudu kulingana na uwezo wao, jambo lilopelekea
kucheza vizuri zaidi ya wapinzani wao.
Turudi kwa Pogba, kiungo mwenye thamani ya £89m anayeifanya United
icheze vyema sana …. anapopangwa mahala ambapo kunaendana na uwezo wa
kipaji chake. Pale Wembley, alikuwa akicheza kwenye safu ya viungo
wawili – akicheza pembeni ya Nemanja Matic – lakini, akiwa na miaka 24
hivi sasa, Pogba bado hajawiva kwenye kuwa na nidhamu kwenye ulinzi ili
kuweza kucheza kwenye nafasi hiyo vizuri. Hivyo pindi anapochezeshwa
kwenye mfumo wa viungo wawili anakuwa tatizo hasa pindi timu yake
inapocheza dhidi ya timu bora.
Matamanio yake ya kwenda kucheza mbele zaidi hayaepukiki na mara zote
amekuwa akipanda mbele na kumuacha Matic pekee yake na walinzi wakiwa
hawana ulinzi wa kutosha, na hili lilionekana dhidi ya safu kali ya
ushambuliaji ya Spurs, ambao waliishinda mechi ndani ya nusu saa tu ya
mchezo.
Kama kiungo wa kati wa hadhi ya Pogba – anatakiwa kuwa na uwezo wa
kuwa na umakini mkubwa ili kuweza kucheza kwa jukumu la kuzuia endapo
atatakiwa kufanya hivyo kutokana na mazingira.
Lakini hawezi kufanya
hivyo, hilo limeshaonekana na sasa ni wazi ni ubishi wa Mourinho
kubadili mbinu na sio kumtuma mchezaji wake staa kufanya kazi ya kuzuia
mashambulizi dhidi ya wachezaji aina ya akina Dele Alli na Christian
Eriksen.
Baada ya kuona Pogba akishindwa kutimiza maagizo aliyompa pamoja na
kujaribu mara kadhaa kwa zaidi ya saa 1 ya mchezo – Mourinho aliamua
kumtoa Pogba na kumuingiza Fellaini.
Chini ya Mourinho, baadhi ya wachezaji wamekuwa wakipewa ulinzi
kuliko wengine – mmoja wao ni Pogba, lakini jana hali ilikuwa tofauti. .
Kutolewa katika mchezo dhidi ya Spurs baada ya kucheza kwa dakika 60,
muda mfupi baada ya kuonekana akisemeshana kwa nguvu na Mourinho katika
kipindi cha kwanza – kwa Pogba hili jambo zuri. Tangu aliporejea United
akitokea Juventus, jana ilikuwa mara yake ya 4 kushindwa kumaliza mechi
ya Premier League ambayo alianza.
Mchezo wa kwanza ulikuwa dhidi ya Crystal Palace mwezi May 2017, hapa
Mourinho alimtoa kwa ajili ya kumuandaa na mchezo wa fainali ya Europa
League vs Ajax, pia mnamo November 2017, akiwa ametoka kwenye majeruhi
Pogba alicheza kwa dakika 70 tu, pia mchezo mwingine ambao hakumaliza ni
ule aliopewa kadi nyekundu vs Arsenal.
Lakini safari hii vs Spurs, Pogba alitolewa kwenye mchezo kwasababu
za kiufundi kama Mourinho alivyoeleza – kwamba alimuondoa kwa kuwa
hakuwa anacheza vizuri. Hata hivyo Mourinho pia hawezi kuepuka lawama.
Kama Mourinho angempanga Ander Herrera pembeni ya Matic na kumtumia
Pogba kucheza mbele yao, kama ilivyokuwa katika mchezo vs Everton mwezi
uliopita wakati Pogba alipocheza kwa kiwango cha juu na kufanikiwa kuwa
Man Of The Match – basi kiungo huyo mfaransa asingechexa vibaya vs Spurs
kwa sababu angecheza eneo analolimudu zaidi kwa ufanisi mkubwa.
Lakini usajili wa Alexis Sanchez, ambaye ameiongezea makali safu ya
ushambuliaji ya United, lakini pia ameleta mkanganyiko wa mbinu na
majaribio ya kulitatua tatizo hilo lilifeli vibaya vs Spurs.
Wakati Pogba akicheza chini, Mourinho alimtumia Sanchez, Martial na Jesse Lingard nyuma ya mshambuliaji wa kati.
Martial na Lingard wameonyesha kwanini wanastahili nafasi katika
kikosi cha kwanza hasa katika mechi za hivi karibuni, wakati Sanchez
ilikuwa lazima aanze lakini watatu hao hawawezi kucheza nyuma ya
mshambuliaji.
Kwanza kwasababu inamuondoa Pogba katika kucheza kwenye nafasi
anayoimudu zaidi – nafasi ambayo anakuwa hatari zaidi kwa timu pinzani
lakini pia inapelekea Mourinho kumpa majukumu mengine ambayo hayaendani
na uwezo wake. Pogba sio mzuri kwenye kufanya ‘tackling’, sio mzuri
kwenye kuzuia mipira ya juu na pia hana uwezo mkubwa wa kugundua hatari
mapema kama ilivyo kwa viungo wa ulinzi. Pia anakosa nidhamu ya kubaki
nyuma.
Kama au endapo Mourinho atafanya usajili wa kiungo mrithi wa Michael
Carrick ambaye atacheza pamoja na Matic, Pogba atakuwa huru kucheza
kwenye kiungo cha kushoto mbele – sehemu ambayo anaimudu vilivyo.
Akileta madhara kwa timu pinzani na uwezo wake wa kuichezesha timu –
akiwa kiunganishi cha nafasi ya ulinzi na ushambuliaji huku akitengeneza
nafasi kwa washambuliaji.
Yote kwa yote, mchezo wa Spurs ulikuwa ukumbusho mwingine kwamba
Pogba sio kiungo mkabaji na Mourinho alifanya makosa kumchezesha kwenye
ulinzi vs Spurs.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.