Waziri
wa Ardhi Maji Nishati na Mazingira Salama Aboud Talib kulia akizungumza
na Ujumbe kutoka kampuni ya CNOOC ya China kuhusiana na masuala
mbalimbali ya Mafuta pamoja na Mafunzo mkutano uliofanyika Ofisini kwake
Forodhani mjini Unguja.
Waziri
wa Ardhi Maji Nishati na Mazingira Salama Aboud Talib wapili kulia
akiwa katika Picha ya pamoja Ujumbe kutoka kampuni ya CNOOC ya China
uliofika Ofisini kwake Forodhani mjini Unguja. kuzungumzia masuala
mbalimbali ya Mafuta pamoja na Mafunzo Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
Na Maryam Kidiko – Maelezo.
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imepokea ujumbe kutoka Kampuni ya Kimataifa ya
China ijulikanayo kama China National Offshore Oil Corporation (CNOOC)
inayojishughulisha na uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia.
Viongozi
wa Kampuni hiyo wamefika katika Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na
Mazingira Forodhani mjini Zanzibar kwa ajili ya kuzungumza mambo mbali
mbali na Viongozi wa Wizara hiyo.
Akizungumza
kuhusu ziara ya CNOOC hapa nchini Katibu Mkuu Wizara ya
Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira Ali Khalili Mirza alisema ujumbe huo ni
utekelezaji wa makubaliano ambayo Kampuni hiyo ilitiliana saini na
Serikali ya Mapunduzi ya Zanzibar.
Katibu
Mirza alisema kampuni hiyo kubwa inayoshuhulikia mambo ya utafiti na
uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia, imekuja kwa lengo la kushirikiana na
Serikali ya Zanzibar katika suala hilo.
Alifahamisha
kuwa katika hati ya makubaliano waliyoawekeana saini na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Kampuni hiyo itafanya kazi zake Zanzibar sambamba
na kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa wataalamu wa Zanzibar
wataoshughulika na sekta ya Gesi na Mafuta.
Aidha
Wataalamu hao kutoka Zanzibar pia watapata nafasi ya kwenda nchini
China kupata mafunzo zaidi kuhusiana na Mafuta na gesi asilia.
“
kampuni ya (CNOOC) imeweza kuonana na Waziri na wamekuja hapa kuweza
kusalimiana nae kama nyumbani na baadae wataweza kuonana na viongozi
mbali mbali wanaohusika na sekta ya Mafuta na Gesi ”alisema Katibu Mkuu.
Kuhusu
hatua ya uchimbaji wa Mafuta iliyofikiwa hapa Zanzibar Katibu Mirza
alisema bado suala hilo lipo katika hatua ya utafiti na kwamba Wataalamu
watakapomaliza taarifa ya matokeo ya utafiti itatolewa kwa Wananchi.