Daktari
bingwa wa maradhi ya moyo Duniani Ramakanta Panda kutoka Taasisi ya
Moyo ya Asia akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani Wizara ya
Afya kuhusu Kambi ya Matibabu ya Moyo inayotarajiwa kufanywa na Taasisi
hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya mwezi June. Kushoto yake ni
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo.(Picha na Abdalla Omari-Habari
Maelezo Zanzibar).
Waziri
wa AfYa Mahmoud Thabiti Kombo akimkaribisha Daktari bingwa wa maradhi
ya moyo Duniani Dkt Ramakanta Panda alipomtembelea Ofisini kwake
Mnazimmoja Zanzibar kuhusu kambi wanayotarajia kuifanya ya matibabu ya
Moyo mwezi June.
Na Faki Mjaka-Maelezo
Kufuatia
ongezeko la maradhi ya moyo Zanzibar Taasisi ya Moyo ya Asia yenye
makao yake nchini India kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Zanzibar
inatarajia kuweka Kambi ya Matibabu ya Moyo kwa kipindi cha wiki moja.
Kambi
hiyo inatarajiwa kuanza mwezi wa Juni ambapo Wataalam wa Tiba za Moyo
watakuja na kufanya uchunguzi wa afya kwa Wananchi wa Zanzibar.
Akizungumza
na Waandishi wa habari Waziri wa Afya wa Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo
amesema kwa wastan Wizara ya Afya inapokea wagonjwa wa Moyo 160 hadi 180
kwa mwaka.
Amesema
idadi hiyo ni ya Wananchi ambao hujitokeza kwa hiari kupima afya zao na
kwamba kuna uwezekano idadi kuongezeka siku hadi siku.
“Hawa
wagonjwa 160-180 tunaowabaini na maradhi ya moyo ni wale tu ambao
wamekuja kupima inawezekana ikawa kuna idadi kubwa ya wagonjwa ambao
bado hawajaenda Hospital kupima afya zao” alisema Waziri Kombo.
Waziri
Kombo amesema wagonjwa watakaobainika na maradhi ya Moyo watafanyiwa
matibabu na wale watakaolazimika kufanyiwa upasuaji watapewa maelekezo
ya wapi waafanyiwe upasuaji.
Amesema
nchini India wagonjwa wengi hawalazimiki kufanyiwa upasuaji badala yake
hupatiwa Dawa kwa vile tu wanawahi mapema kufanyiwa uchunguzi wa
kiafya.
Hivyo
Waziri huyo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao kwa
wastani wa mara moja kwa mwezi ili kujiweka katika mazingira mazuri
kiafya.
Kwa
upande wake Daktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Asia
Ramakanta Panda amesema kwa kipindi cha mwaka Taasisi yao itatuma timu
ya wataalam wa maradhi ya Moyo kuja Zanzibar kufanya kambi mara mbili
kwa lengo la kukagua afya za Wagonjwa wa Moyo Unguja na Pemba.
Mbali
na Kambi, Taasisi hiyo imekubali kuwasomesha Madaktari wawili kutoka
Zanzibar ambao wataenda nchini India kujifunza zaidi kuhusu maradhi ya
Moyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Dkt.
Panda amesema yupo tayari kushirikiana moja kwa moja na Serikali ya
mapinduzi ili kusaidia ujenzi wa kituo cha matibabu ya Moyo maeneo ya
Binguni Wilaya ya Kusini Unguja.
Aidha
Waziri Kombo amemuonesha Dkt. Bingwa huyo michoro mbali mbali ya kituo
cha Taasisi ya Moyo Zanzibar ambacho kitasaidia pakubwa katika mapambano
dhidi ya maradhi ya Moyo.
Madakatari
hao watakuja kufanya uchunguzi wa Moyo kwa wananchi mbali mbali kupitia
vifaa mbali mbali na kutoa ushauri wa kitaalamu namna bora ya kujikinga
na maradhi mbalimbali ikiwemo Moyo.