HABARI KUU
Katika moja ya mkutano na waandishi wa habari ambao
ulionekana kugubikwa na hisia sana ni usiku wa kuamkia leo wakati
Antonio Cinte akizungumza baada ya mchezo wao dhidi ya Watford
kumalizika.
Chelsea walidhalilika tena kwa kupigwa bao 4 kwa 1 jambo ambalo
limeendelea kuwasha moto Stamford Bridge na sasa kocha wao Antonio Conte
yuko katika kitimoto huku hatma ya kibarua chake ikiwa kwa Roman
Abromovich.
Lakini Conte yeye amesema suala la kazi anawaachia mabosi wake kwani
yeye binafsi amekuwa akijitoa kwa 120% kwa ajili ya timu hiyo na
kinachotokea uwanjani ndio kama hivyo kinavyoonekana.
Conte amesema kuhusu kibarua chake yeye anaona yuko poa tu na Chelsea
lakini kama wenyewe Chelsea wataona kwamba hafai kuendelea kukaa
klabuni hapo baasi ataondoka tu lakini hana wasiwasi.
Antonio Conte amesisitiza kwamba yeye hakoseshwi usingizi na tetesi
za kufukuzwa kazi na amesema yeye anaona anafanya vizuri kwa ajili ya
Chelsea ila kama wataona vinginevyo baasi watafanya lililo sahihi.
Conte inasemekana alijaribu kuongea na uongozi wa Chelsea kabla ya
mchezo wao na Watford kuhusu kujaribu kuongea na wanahabari kuhusu
uhakika wa kibarua chake lakini Chelsea hawakuwa tayari kwa sasa
kuongelea hilo.
Mara ya mwisho kwa Chelsea kukubali kipigo mfululizo cha mabao 3+
katika EPL ilikuwa mwaka 1995 walipopigwa na United 1-4, kisha wakapigwa
na Blackburn 0-3, kwa hiyo jana inakuwa mara ya kwanza kufanywa hivyo
tangu 1995.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.