Haina ubishi kwamba kwa sasa kati ya makocha wenye vibarua vigumu hivi sasa ni Antonio Conte, kipigo usiku wa leo mbele ya Watford kinaweza kuwa hitimisho la uvumilivu wa Roman Abromovich.
Chelsea waliokuwa pungufu walianza kutungulia dakika ya 42 ya mchezo kwa goli la penati la Troy Deeney ambaye sasa anakuwa amefunga penati sawa na Harry Kane na Kun Aguero (12) katika EPL tangu 2015.
Dakika ya 82 Eden Hazard aliisawazishia Chelsea waliokuwa pungufu baada ya Tiemoue Bakayoko kuoneshwa kadi nyekundu na kuonekana kama mpira utaisha kwa suluhu lakini dakika 2 baadae Daryl Janmaat aliongeza bao la 2 kwa upande wa Watford.

Kama ulikuwa hujui tu ni kwamba mara ya mwisho kwa Chelsea kupoteza michezo miwili kwa mabao 3+ ilikuwa miaka 22 iliyopita na kipigo cha hii leo kinafanya jambo hilo kujirudia tena.