HABARI KUU
Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma amewataka wananchi kuchukua hatua
dhidi ya maofisa wa Mahakama wanaokiuka maadili ya kazi na
wanaojihusisha na vitendo vya rushwa badala ya kulalamika.
Pia, ametaka wananchi kutambua wanapokwenda mahakamani si lazima
washinde ndipo waone haki imetendeka kwa kuwa uamuzi wa Mahakama ni
mchakato unaopitia mtiririko maalumu.
Profesa Juma amesema hayo leo Jumapili Januari 28,2018 alipozindua
Wiki ya Sheria katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
“Mahakama inawathamini wananchi. Tumeweka matangazo kwenye
ngazi mbalimbali za Mahakama ambayo yanaonyesha namba za simu za wote
wanaohusika,” amesema.
Profesa Juma amesema, “Kama mwananchi akiona hatendewi haki
labda anaombwa rushwa, badala ya kulalamika tu atumie namba zile za simu
kupiga kwa mamlaka husika, hasa Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa) ambao ndio wanahusika na suala hilo.”
Alisema, “Mwananchi akiwa analalamika tu bila kuchukua hatua hawezi kuisaidia Mahakama, kwa hiyo waanze kuchukua hatua.”
Amewataka watumishi wa Mahakama na watoa haki kuwa na maadili mema na
kutojihusisha na vitendo vya rushwa ili wananchi wawe na imani na
Mahakama.
Jaji mkuu amesema kumekuwa na dhana kuwa mtu anapokwenda mahakamani ni lazima ashinde ndipo anaona kuwa haki imetendeka.
Amesema ili haki ipatikane kuna mlolongo wa hatua na utaratibu wa
kufuata na la msingi ni mtu kusikilizwa ndipo Mahakama inatoa uamuzi.
“Sasa maamuzi yanayotoka si lazima wewe ushinde, huo ndio
msingi wa haki. Wananchi wengi wanadhani kwamba wakienda mahakamani ni
lazima tu washinde,” amesema.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.