Shirika la Umeme Zanzibar ZECO
limekusudia kuimarisha huduma ya Nishati ya Umeme kwa wananchi ili
kuwaondoshea usumbufu wanaokumbana nao wakati wakihitaji huduma hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari baaada
ya Kufunga mafunzo ya Siku tatu kwa taasisi Zinazosimamia Nishati
Zanzibar, Meneja Mkuu wa Shirika hilo Hassan Ali Mbarouk amesema
kutokana na mafunzo waliopewa wasisimamizi wa taasisi za Nishati
,wataweza kutoa huduma Bora kwa wananchi.
Amesema katika mafunzo hayo wamejifunza
namna Bora ya Ununuzi na Njia sahihi ya kuuunganisha Mitandao ya Shirika
hilo kwa Mfumo maalum kupitia Mita za tukuza katika kipindi cha miaka
miwili ijayo .
Pia watawewezesha watowa huduma na kujua
namna ya kuwahudumia wateja wao ili waweze kuzuia mapato ya serikali
yasipoteee katika manunuzi .
Kwa upande wake Afisa Mdhamini wa Wizara ya
Ardhi Maji Nishati na Mazingira Pemba Juma Bakari Alawi amesema ili
mafunzo hayo yaweze kufikia malengo waliyokusudiwa ni vyema kwa wananchi
kuendelea kulipia huduma hiyo bila kushurutishwa ili kuliwezesha
Shirika la ZECO kuweza kutoa huduma ya Nishati kwa wananchi.
Amesema ZECO ni shirika linalojitegemea
katika kutoa huduma kwa wananchi hivyo wananchi kutolipia huduma hiyo na
wakati na kwa kufuata sheria kusababisha kuzorota kwa huduma hiyo.
Semina hiyo ya Siku tatu iliyofanyika
kilimani Mjini Zanzibar imeshirikisha wadau mbali mbali wa shirika hilo
Wakiwemo Viongozi wa Bodi ya ZECO pamoja na watendaji wa Wizara ya Ardhi
,Maji ,nishati na Mazingira ikiwa na lengo la kujifunza namna ya
kuimarisha utoaji wa huduma ya Nishati kwa Wananchi.