
Wizara ya mambo ya nje ya China imetangaza kuwa, kutokana na mialiko, rais Xi Jinping wa China atafanya ziara ya kiserikali nchini Hispania, Argentina, Panama na Ureno kuanzia tarehe 27 mwezi huu hadi tarehe 5 mwezi ujao.
Katika kipindi cha ziara hiyo, rais Xi Jinping atahudhuria mkutano wa 13 wa kilele wa kundi la nchi 20 utakaofanyika kuanzia tarehe 30 mwezi huu hadi tarehe 1 mwezi ujao mjini Buenos Aires.