
HABARI KUU
Baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia nchini Urusi, akili ya watu wengi kwa sasa ipo kwenye michuano mbalimbali ya ligi kuu Duniani.
Wakati nchi mbalimbali zikiendelea kufuatilia ligi hizo na michuano mbalimbali, Qatar wao wapo bize wakifanya maandalizi ya michuano hiyo ya kombe la dunia kwa ajili ya kivumbi hicho mwaka 2022.
Tayari Qatar wameanza kuonesha maendeleo yao hasa katika suala la viwanja ambavyo vitatumika kwa ajili ya michuano hiyo. Kwa mara ya kwanza michuano hiya inatarajiwa kuanza kufanyika Novemba 21 na kumalizika Desemba 18.
