Mbwa aliyekuwa amepewa kazi ya kuwa msaidizi wa rais wa zamani wa Marekani George HW Bush amepigwa picha akionekana kuomboleza karibu na jeneza la kiongozi huyo.
Bw Bush, aliyehudumu kama rais wa 41 wa Marekani kati ya mwaka 1989 na 1993 alifariki dunia Ijumaa usiku akiwa na miaka 94.
Sully, mbwa wa jamii ya golden labrador, alisafiri pamoja na mwili wa marehemu kwenye ndege kutoka Texas kwenda Washington DC siku ya Jumatatu.
- George HW Bush alikuwa mtu wa aina gani?
- 'Zawadi ya amani' kutoka kwa Kim Jong Un kwa Korea kusini
- Putin akataa zawadi ya mbwa kutoka Japan
Jeneza lenye mwili wake lilisafirishwa kwa ndege kutoka Texas kwenda DC kwa ndege ya Air Force One - ambayo kwa muda ilipewa jina Special Air Mission 41, kwa heshima ya rais huyo.
Mwili huo ulirejeshwa Texas Jumatano.
Mbwa huyo wa jina Sully alisindikiza jeneza hilo muda wote.
Picha ya kwanza kabisa ya Sully akitoa heshima zake ilipakiwa mtandaoni na msemaji wa Bw Bush Jim McGrath, pamoja na ujumbe: "Mission complete."
Watu katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakimshukuru Sully kwa huduma zake, na kwa kawaida kuzungumzia uaminifu wa mbwa kwa wamiliki wao.