
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, amesema kuwa anachotambua uchaguzi wa Yanga unafanyika Januari 1 mwakani na wa kujaza nafasi za viongozi waliojizulu.
Mwakyembe amesema klabu ya Yanga haiwezi ikaendeshwa bila ya kuwa na uongozi hivyo ni wakati mwafaka wa kufanyika kwa uchaguzi ili kujaza nafasi zote zilizo wazi.
Waziri huyo mwenye dhamana ya michezo amekanusha taarifa zinazosema kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kuwa amerejea kwenye nafasi yake akieleza ni taarifa za vijiweni na hawezi kuzingumzia.
Aidha, Mwakyembe amefunguka kuwa tayari wameshamaliza taratibu zote na Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na akieleza mengine TFF watakuwa wanahusika kuyajibu.
"Tumeshamaliza taratbu zote na TFF, BMT na Yanga, hayo mengine yanayozungumzwa siwezi kuyasemea chochote mimi kwa maana si taarifa rasmi, ninachojua uchaguzi uko palepale kama ilivyopangwa" alisema Mwakyembe.