Hayo aliyazungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji uliodhaminiwa na Direct Aid huko Muungoni Wilaya ya kusini Unguja.
Aidha Kitwana amesema visima hivyo vimechimbwa wakati muhimu ambao kijiji cha Muungoni kina shida ya huduma ya maji kutokana na kuharibika tangi la mtule hivyo Direct Aid wameweza kusaidia huduma hiyo muhimu ya Maji ili kuondosha usumbufu unaojitokeza ndani ya kijiji hicho.
‘’Kuyatunza maji ni gharama sana hivyo hatuna budi kuutunza huduma hii muhimu ni neema kwetu sote mungu atakwenda kutuuliza kesho neema hii tuliopatiwa na tutajibu ‘’ Alisema Idrissa Kitwana.
Hata hivyo ameiomba kamati ya kijiji hicho kuondosha dhana ya umiliki wa mtu mmoja wa visima hivyo na kuwacha kuvitumia kwa maslahi yao kinyume na utaratibu.
Kwa upande wake Mkuregenzi mkuu wa Shirika la Direct Aid Aiman Mohamed Kamal Din amesema kwa sasa wamejipanga kuhakikisha wanawasaidia huduma ya umeme ili kuwezesha visima hivyo vinne viweze kuendelea kutumika bila ya vikwazo.
Risala ya wanakijiji wa kijiji hicho cha Muungoni wamelipongeza Shirika hilo kwa kuwaletea huduma hiyo muhimu na kuahidi kuitunza ili iweze kuwaletea manufaa baadae.
Wamesema visima hivyo vitasaidia zaidi ya waakaazi 1000 na kuwapunguzia mzigo wa kwenda masafa marefu kutafuta huduma ya maji Safi na salama.
Jumla ya visima vinne vya kisasa vimechimbwa na Shirika hilo kwenye kijiji cha Muungoni na vimegharimu jumla ya TSH 22,000,000.