Marekani yapitisha sheria inayo iwajibisha DRC - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, November 30, 2018

Marekani yapitisha sheria inayo iwajibisha DRC

Sheria ya 2018 inayo iwajibisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuheshimu haki za binadamu na kuendeleza demokrasia imepitishwa Jumanne na Bunge la Marekani. Sheria hiyo inaweka pia vikwazo dhidi ya serikali inayo kaidi agizo hilo. Pia inaitaka serikali ya DRC kuwaachia wafungwa wote wa kisiasa, kuondoa vipingamizi vya uhuru wa kujielezea, vyombo vya habari, kukusanyika na kujiunga na chama chochote, kuheshimu haki ya kuandamana kwa amani na kuhakikisha vyombo vya usalama vinawajibishwa kwa vitendo vya unyanyasaji ilivyo fanya. Mbunge wa Chama cha Demokrat Karen Bass mwenye nafasi ya juu katika chama chake akiwa ni mjumbe wa Kamati ndogo ya Mambo ya Nje ya Baraza la Wawakilishi inayoangaza Afrika, ametoa tamko baada ya kupitishwa sheria hiyo. “DRC ina fursa ya kuwa nchi tajiri kuliko zote duniani, lakini imeathiriwa na miongo mingi ya vita na ufisadi,” amesema mbunge huyo Bass. Wananchi wa DRC kwa muda mrefu wamekuwa wakiiomba jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua ya kukiwajibisha chama tawala kuheshimu katiba ya nchi yao. Sheria hii inakidhi maombi yao na inapeleka ujumbe kwa ulimwengu mzima kuwa Marekani haijarudi nyuma katika ahadi yake ya kulinda haki za binadamu na kuendeleza demokrasia ulimwenguni, ameandika Bass

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI