Vicensia Shule: Aliyekuwa na ujumbe wa Magufuli aitwa kamati ya maadili - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, November 30, 2018

Vicensia Shule: Aliyekuwa na ujumbe wa Magufuli aitwa kamati ya maadili

HABARI KUU Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) aliyezua mjadala mtandaoni baada ya kudai kwamba rushwa ya ngono imekithiri chuoni humo ameitwa kufika kwenye kamati ya maadili ya chuo hicho. Dkt Vicensia Shule alikuwa ameandika kwenye Twitter kwamba alitaka sana kuufikisha ujumbe wake kwa Rais John Magufuli lakini aliwaogopa walinzi wake. Dkt Magufuli alikuwa amezuru chuo hicho kufungua maktaba mpya, kubwa na ya kisasa ya Kikuu cha Dar es Salaam iliyojengwa katika Kampasi Mlimani (Mwalimu. Julius K. Nyerere) jijini Dar es Salaam. Mhadhiri aliyetaka kufikisha ujumbe kwa Magufuli UDSM Dkt Shule alitaka kutumia bango kuufikisha ujumbe kwa rais huyo. Aliandika: "Baba @MagufuliJP umeingia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kufungua maktaba ya kisasa. Rushwa ya ngono imekithiri mno UDSM. Nilitamani nikupokee kwa bango langu ila ulinzi wako umenifanya ninyamae. Nasubiri kusikia toka kwako maana naamini wateule wako ni waadilifu watakwambia ukweli." Alhamisi jioni, aliandika kwenye Twitter kwamba amepigiwa simu na kutakiwa kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya UDSM. "Leo Alhamisi 29 Nov jioni nimepigiwa simu kuitwa kwenye Kamati ya Maadili siku ya Ijumaa 30 Nov mchana. Nasubiri mwaliko rasmi kwa maandishi," aliandika. "Kwa manusura wa udhalilishaji huu wa kingono, tunakaribia kufika, tutashinda, tutapata ushindi mkubwa!" Haki miliki ya pichaTWITTER Ingawa hakueleza ni rushwa ya aina gani iliyokithiri, katika vyuo vikuu vingine kumekuwepo na tatizo la wahadhiri na wanafunzi kutumia ngono katika kutoa alama katika mitihani. Mtanzania aliyetengeneza helikopta aunda gereji la kuhama hama Aidha, baadhi ya wahadhiri hutuhumiwa kudai ngono kutoka kwa wenzao ndipo wawapandishe vyeo vyuoni. Tamko lake lilizua mjadala mtandaoni, baadhi wakikubaliana naye na wengine kumwambia angetumia tu ujasiri na kutimiza azma yake.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI