Naibu Waziri wa Wizara hiyo Hassan Khamis Hafidhi amesema lazima wafanyabiashara watekeleze agizo la serikali la kushusha bei ya bidhaa ikiwemo Mchele, Sukari, Unga wa ngano na Tende kwani tayari serikali imewaondoshea kodi kwa bidhaa hizo wanapoingiza nchini.
Bei elekezi zilizopangwa na Serikali kwa bidha hizo ni:
- Sukari Kilo isizidi Tsh. 1700/= kwa Zanzibar, na Tsh.1800/= kwa Pemba
- Unga wa ngano kilo usizidi Tsh.1100/=
- Tende kilo Tsh.3000/= na
- Mchele kilo Tsh.1250/=
Hafidh amesema endapo wafanyabiashara hao watakaidi agizo hilo na tayari serikali imetoa bei elekezi hatua za kisheria zitachukulia dhidi yao kwani wanawapa usumbufu wananchi ambao wanahitaji bidhaa hizo.
Aidha amewataka wananchi kutoa taarifa mda wowote watakapoona mabadiliko yoyote katika bei za bidhaa ili kuweza kuchukuliwa hatua hao wanaokaidi amri ya serikali.
Naibu waziri huyo pia ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya Zanzibar pamoja na Masheha kushirikiana na wananchi katika kuwabainisha hao wafanyabiashara wanaopandisha bei katika mwezi huu mtukufu.
Hata hivyo amewaomba wafanyabiashara wa mazao na wao kupunguza bei bidhaa zao katika mwezi huu ili wananchi nao waweze kumudu gharama za bidhaa hizo hususani Muhogo,Ndizi,Nazi,Majimbi,Viazi na bidhaa nyengine muhimu.
Amina Omar