Burundi imesitisha matangazo ya vituo vya kimataifa vya radio za Uingereza na Marekani, BBC na Voice of America VOA, kabla ya kura ya maoni inayotarajiwa tarehe 17 mwezi huu, inayolenga kurefusha muhula wa Rais Pierre Nkurunziza hadi mwaka 2034.
BBC na VOA zinadaiwa kukiuka sheria za vyombo vya habari na kuendesha shughuli zao kinyume na maadili. Radio France International, kituo cha Burundi cha Isanganiro na CCIB FM pia zimeonywa.