Vinay Kumar ni mwanasayansi wa hifadhi ya wanyama pori katika jamii ya watu wa India,alipiga picha ya video ya sekunde 48 wakati yuko katika safari ya kikazi katika msitu wa Nagarhole katika mji wa Karnataka mwezi april mwaka 2016.
Aliwaambia BBC kutoionyesha video hiyo mpaka sasa kwa sababu hakutambua umuhimu wa video hiyo sana.
Wanasayansi wanasema mpaka sasa hawaelewi ni kwa nini tembo huyo alikuwa anatoa majivu.
- Xdolls: Vyumba vya midoli ya mapenzi vinavyozua mjadala Paris vyanusurika
- Maajabu ya viumbe wenye vichwa viwili
Hifadhi ya wanyamapori nchini India inasema hii ni video ya kwanza inayoonyesha Makala ya tembo akionyesha tabia ya namna hiyo,jambo ambalo limewaacha na bumbuwazi wanasayansi pamoja na wataalamu wa wanyama pori.
Bwana Kumar amesema yeye na wenzie walitembelea katika msitu huo nyakati za asubuhi ili kuona kama camera zao walizoziweka zimewapiga picha chui.akini wanakuta imempiga picha tembo wa kike aliyekuwa katika umbali wa mita 50 wa kamera.
Tembo huyo alionekana akitoa makaa na kuacha moto chini pindi majivu hayo yanapomtoka.
Kile tulichokiona ni sawa na kuona tembo huo akivuta ,alikuwa anatoa majivu mengi kutoka katika katika mdomo wake na kutoa moshi huo kama alikuwa anavuta.
Mtaalamu wa tembo Varun Goswami,alichunguza video hiyo na anaamini kuwa inawezekana tembo huyo alikuwa anatoa moto wa makaa,kwa sababu alionekana kama anatoa kitu kutoka chini,na kupuliza majivu yaliyokuwa pamoja nayo na kusababisha afanye hivyo
Aidha alisema mkaa unajulikana kuwa una athari ingawa unawea kuwa hauna virutubisho vingi,wanyama pi wanaweza kuvutiwa nao kwa ajili ya tiba.