Rais pekee wa kike barani Afrika, rais wa Mauritius, Ameenah Gurib-Fakim angali anakabiliwa na shinikizo kwamba ajiuzulu.
Bi.Gurib-Fakim amekuwa akituhumiwa na kashfa ya matumizi mabaya ya fedha.
Bi.Gurib amekuwa akikanusha madai hayo ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kutoka shirika lisilo la kiserikali fedha ambazo zilinuiwa kusaidia katika ada za wanafumzi kutoka jamii maskini.
Anasemekana alizitumia kwa ajili ya matumizi yake binafsi ya nguo na vitu vingine vya thamani.
- Rais pekee wa kike barani Afrika ataachia ngazi
- Rais mwanamke aliyebaki Afrika akataa kunga'tuka
- Jacob Zuma akabiliwa na mashtaka ya rushwa
Lakini siku moja baada ya kukataa wazo la kujiuzulu wakili wake Yusuf Mohamed aliwaambia waandishi wa habari wa nchi hiyo kuwa rais huyo huenda atajiuzulu.
Waziri mkuu wa nchi hiyo alisema rais huyo angeachia wadhifa wake Jumatatu iliyopita, jambo ambalo halikufanikishwa .
Bi Gurib amekuwa akisema fedha hizo alizirudisha na hivyo hana kosa lolote.