Na Haji Manara
Watu wengi huwa hawajui tunapopoteza mechi na hunitokea, lakini leo imebidi niwe wazi kwa wanasimba wenzangu, Mke wangu, Rais wangu Evans Aveva na anayekaimu kwa sasa Salum Abdallah wanajua Simba ikifungwa au kutoka sare katika mechi nyepesi naishia kulia tu.
Nitalia kama mtoto mdogo wakati mwingine kilio changu kinaambatana na kwiki kama nimefiwa na Baba au Mama"
"lakini kwa sare ya jana dhidi ya Al Masry sijaashungusha hata tone la chozi.
Sanasana nilimshukuru Mungu na kujisemea moyoni kuwa mm ni msemaji wa Timu bora sana ktk Afrika Mashariki. Yes kupata sare pacha ugenini pale Bourj Saiid (port side) na timu bora kama Al Masry tena mbele ya maelfu ya mashabiki wao baada ya kukaa nje kwa miaka mitano kwenye CAF Competition ni kujivunia kunakostahili, no matter kuwa hatukufuzu kwa next round"
"Ikumbukwe Al Masry waliwapiga Green Buffalo ya nchini Zambia goli nne kwa bila ktk mzunguko wa awali wa kombe la Shirikisho.
Lakini why sijaangusha chozi Jana usiku? Sababu wachezaji walipigana kwa nguvu zao zote. niliiona fighting spirit ya jasho na damu. niliiona hassle ya Wanaume ndani ya dimba.
Kifupi nilimuona Juuko ninayemjua, Aishi Tanzania one. Nilimuona Mkude halisi nilimuona Erasto aliyekunja uso dakika tisini lakini niliwaona wapiganaji bora zaid kuwahi kutokea ktk kipindi cha miaka Sita nyuma ya uhai wa Simba."
"Usisahau mbinu sahihi za Mwalimu Lechantre ambae aliamua kufunguka second half na kuwafanya waarabu waombe game iishe..ahhh mechi kama hzi ztabaki kwenye vichwa vya watanzania kwa siku nyingi zijazo."
"Asubuhi hii likanijia swali moja. hv kwa kiwango na aina ya uchezaji wa Simba tunastahili eti kupata sare na Stand au Mwadui. au hata kukaribiana points na Yanga niliyoiona Jana pale Botswana?
Yanga hii iliozidiwa ball possession na timu kama Lipuli, Majimaji, Ndanda na hata Ruvu Shooting?"
"Kwa msimu huu ntaamini mpira Haraam kama wanaume wale wa Jana watashindwa kuifunga Yanga na kuchukua ubingwa wa VPL.
Nitawaambia kweupe wachezaji, kwa ubora mlio nao mkishindwa kutupa ubingwa nitawaandika kwa kalamu ya wino wa damu kwenye moyo wangu. sio tu kwamba ntawachukia ila ntauchukia mchezo wa Soka na ntakaa pembeni kujihusisha na mchezo huu ulionisaidia kunikuza, kunilea na kunisomesha.
Mimi ni mtu wa misimamo na ntalisimamia hilo kwa kiapo cha watoto wangu."
Nimalizie kwa kuwashukuru wanasimba wenzangu ambao always dua na sala zenu mnatuombea. nyie ni kumbukizi bora niliyowahi kukutana nayo ktk maisha yangu, hakika watu wa Simba ni watu wa Soka. ni watu timamu, ni watu weledi na mnaifanya Simba kuwa Super football club nchini.
Mbarikiwe sana".