Ujumbe kutoka Wizara ya Fedha na Mipango ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto), wakifuatilia mazungumzo kati yao na ugeni kutoka Benki ya Barklays nchini Afrika Kusini (hawako pichani), mkutano uliofanyika mjini Dodoma
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akizungumza
wakati wa mkutano kati yake na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
Barclays Afrika, Bw. Peter Matlare (hayupo pichani), kuhusu namna ya
kuboresha ushirikiano katika kukuza biashara kati ya Tanzania na benki
yake,uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.
Ujumbe kutoka Benki ya Barclays uliongozwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika, Bw. Peter Matlare (kulia), wakichukua kumbukumbu wakati wa mkutano kati yao na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mijini Dodoma.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika Bw. Peter Matlare akielezea
umuhimu wa kushirikiana katika kukuza biashara na uwekezaji kati ya
Tanzania na Benki yake wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani)
uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.
Maafisa Wakuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakichukua kumbukumbu wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika Bw. Peter Matlare (hawapo pichani), uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akipeana mkono na Makamu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika Bw. Peter Matlare, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tano kulia), Makamu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika Bw. Peter Matlare (wa
sita kushoto) wakiwa katika picha yapamoja na baadhi ya Watumishi wa
Wizara ya Fedha na Mipango na Benki ya Barclays baada ya kumalizika kwa
mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akiagana na Makamu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika Bw. Peter Matlare, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Sera), Dkt. Khatibu Kazungu,
akibadilisha mawazo na naimbu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays
kundi la Afrika, Bw. Peter Matlare, baada ya kumalizika kwa mazungumzo
ya Wizara ya Fedha na Uongozi wa Beni hiyo kutoka Afrika Kusini, Mjini
Dodoma
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
Benny Mwaipaja, Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, amekutana na Naibu Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Barclays Kanda ya Afrika, Bw. Peter Matlare na
kuiomba Benki hiyo kuangalia uwezekano wa kutoa mkopo nafuu wa ujenzi wa
miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali ukiwemo ujenzi wa Reli ya
Kati kwa viwango vya kimataifa (SGR) mradi wa miundombinu ya umeme wa
Stieglar's Gorge ili kurahakisha maendeleo ya kiuchumi kupitia viwanda.
Amemweleza
kiongozi huyo kwamba Serikali imeimarisha uchumi Mkuu kwa kudhibiti
mfumuko wa bei ambao uko katika kiwango chatarakimu moja cha wastani wa
asilimi 5.3 katika kipindi cha miezi 6 iliyopita.
"Tumewekeza
kwenye miundombinu kama vile Elimu, maji, kilimo, afya, madini, na
biashara na kwamba katika kipindi kifupi cha miaka 2 zaidi ya viwanda 80
vimejengwa katika eneo la Mkuranga mkoani Pwani, kutokana na fursa za
uwepo wa bomba la gesi na eneo hilo kuwa karibu na Bandari ya Dar es
Salaam.
Dkt.
Mpango ameelezea pia mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha
Kimataifa (SGR) ambao amesema utarahisisha usafiri na usafirishaji wa
abiria na mizigo katika nchi zinazopakana na Tanzania hivyo kukuza
biashara kwa kiwango kikubwa.
Akizungumzia
kuhusu ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme katika Bonde la mto Rufiji
(Stiegler's Gorge), Dkt. Mpango amesema lengo la mradi huo utakao
zalisha megawati 2,100 za umeme utakao kuwa wa uhakika na bei nafuu ili
kukuza viwanda.
Alisema
kuwa mwelekeo wa Serikali kwa sasa ni kuhakikisha kuwa kila biadhaa
zinazozalishwa nchini pamoja na madini, vinaongezwa thamani hapa hapa
nchini badala ya kuuzwa kama malighafi na kwamba nishati ya umeme ndiyo
nguzo kuu ya kufikia malengo hayo.
"Ili
tuweze kufikia azma hiyo tunahitaji kuwa na umeme wa uhakika na wa bei
nafuu ili viwanda vyetu viweze kuzalisha kwa wingi ndio maana tunaiomba
Benki yako iweze kufikiria namna ya kushiriki katika ujenzi wa miradi
hii" Alisisitiza Dkt. Mpango.
Dkt.
Mpango ameipongeza Benki ya Barclays ambayo pia ni mwanahisa katika
Benki ya NBC kwa ahadi yake ya kutaka kuwekeza kiteknolojia katika sekta
ya benki nchini hatua ambayo itasaidia kukuza mitaji na mikopo kwa
kundi kubwa la watanzania wakiwemo wajasiriamali wadogo, wa kati na
wakubwa.
Alielezea
msimamo wake kwamba katika kukuza uchumi, Serikali inathamini mchango
mkubwa wa Sekta Binafsi na imeendelea kuweka mazingira mazuri ya
uwekezaji na kwamba hivi karibuni alikuta na wadau wa Sekta ya Benki ili
kusikiliza changamoto zao na pia kuwaeleza mambo muhimu ambayo
ingependa sekta Binafsi ifanye ili kufikia malengo yanayokusudiwa.
Awali,
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ya Barclays anaye hudumia kundi
la benki za Barclays Barani Afrika na kwingineko Marekani na Ulaya, Bw.
Peter Matlare, ameipongeza Serikali chini ya Rais Dkt. John Magufuli
kwa kusimamia kikamilifu uchumi wa nchi unaokua kwa wastani wa asilimia
7.
Alisema
hatua hiyo ni ya kupigiwa mfano katika nchi za Kiafrika na Duniani kwa
ujumla ambapo amesema Tanzania imekuwa ikifanya vyema katika kukuza
uchumi jumuishi unaowafikia watu wengi zaidi wakiwemo waishio mijini na
vijijini.
Bw.
Peter Matlare amemhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip
Mpango, kwamba Benki yake itayafanyia kazi mapendekezo ya kutaka
ushiriki wake katika ujenzi wa miradi mikubwa iliyoainishwa na Serikali
kuwa kipaumbele chake.