HABARI KUU
Kulikuwa na mashaka juu ya uandaaji wa michuano ya AFCON
mwaka 2019 ambapo nchi ya Cameroon ndio wanatari kuwa wenyeji wa
michuano hiyo inayotarajiwa kuanza June 7 hadi July 7 mwakani.
Kulikuwa na taarifa na hofu kwamba Cameroon hawako tayari
kimiundombinu pamoja na kiuchumi kuandaa michuano hiyo mikubwa Afrika na
ilibidi CAF kuanza kuchunguza maandali ya michuano hiyo.
Baada ya uchunguzi huo CAF wametoa ruhusu kwa Cameroon kuendelea
kufanya maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo baada ya timu ya maafisa
wa CAF kuridhishwa na maandalizi yanayoendelea nchini humo.
Juniour Binyam mwenyekiti wa kamati ya
masuala ya habari wa CAF amethibitisha hilo na kusema kwamba CAF kwa
sasa hawana mashaka juu ya maandalizi ya michuano hiyo na wanaona hadi
kufika wakati huo Cameroon watakuwa tayari.
Inatajwa moja ya sababu kubwa iliyokuwa
inatoa mashaka kwa CAF kutowaamini sana Cameroon ni kutokana na ongezeko
la timu kutoka 16 kwenda hadi 24 jambo ambalo ilidhaniwa inaweza
kuwasumbua Cameroon lakini wanaonekana wanaweza kukabiliana nalo.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.