Katibu
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Raya Issa Msellem akizungumza na
Waandishi wa habari kuhusiana na kuanza kwa Mkutano wa tisa wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar (Picha na Kijakazi Abdalla Maelezo)
Na Kijakazi Abdalla - Maelezo Zanzibar 5/02/2018
Mkutano wa tisa wa baraza la tisa la wawakilishi unatarajiwa kuanza siku ya Jumatano ya tarehe 7 Febuari 2018 .
Akizungumza
na Waandishi wa habari huko ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani
Mjini Unguja Katibu wa Baraza la wawakilishi Raya Issa Msellem amesema
kuwa jumla ya maswali 74 yanatarajiwa kujibiwa kwenye mkutano huo.
Amesema
kuwa mbali na maswali hayo pia katika mkutano huo kutasomwa miswada ya
sheria iliyowasilishwa na kusomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa
Disemaba 2017 na itasomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa katika mkutano
huo.
Aidha
alisema kuwa miswada hiyo ni pamoja na Mswada wa sheria ya kufuta
sheria ya kusimamia mwenendo wa biashara na kumlinda mtumiaji ya
Zanzibar Nam 2 ya mwaka 1995 na kutunga sheria mpya ya ushindani halali
wa biashara na kumlinda mtumiaji,kuweka masharti bora zaidi pamoja na
mambo mengine yanayohusiana na hayo.
Pia
alisema kuwa kutakuwa na mswada wa sheria ya kufuta sheria ya adhabu na
kutunga sheria mpya ya adhabu,kuweka masharti bora zaidi pamoja na
mambo mengine yanayohisiana na hayo.
Aidha
alisema kuwa mswada wa sheria ya kufuta sheria ya mwenendo wa jinai
Nam.7 ya mwaka 2004 na kutunga sheria mpya ya mwenendo wa jinai na
kuweka utaratibu bora upelelezi wa makosa ya jinai na usikilizaji wa
kesi za jinai na mambo mengine yanayohusiana na hayo.
Sambamba
na hayo pia alisema kuwa kutakuwa na ripoti za kamati za kudumu za
baraza la Wawakilishi kwa mwaka 2017/2018, na taarifa ya Wabunge watano
(5) wanaoliwakilisha Baraza katika Bunge la Jamuhuri ya Muungano.
Pia
kutakuwepo na Ripoti ya Serikali kuhusu hoja binafsi ya Mjumbe kuhusu
kuweka Miundombinu bora kwa watu wenye Ulemavu katika
majengo,barabara,makaazi maeneo ya kupumzikia na maeneo mengine.
Aidha
alisema kuwa pia kutakuwa na ripoti ya serikali kuhusu maombi ya
wananchi wa Kisakasaka Zanzibar kuhusu namna wanavyoweza kufaidika
kutokana na machinjio ya wanyama yaliyopo maeneo yao.