Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu katikati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana
na Siku ya Sheria Duniani ambapo kwa Zanzibar kitafanyika kilele chake
12-02-2018 katika bustani ya Victoria Mnazi mmoja mjini Unguja. Ujumbe
wa mwaka huu ni Kuimarisha Utawala wa Sheria na Kuimarisha Uchumi
Zanzibar.kulia yake ni Kaimu mrajisi wa Mahkama Yessaya Kayange na
kushoto ni Hakimu wa Mahkama ya Watoto Sabra Ali Mohammed.
Kaimu Mrajisi wa Mahkama Yessaya Kayange akitolea ufafanuzi wa baadhi ya maswali yalioulizwa katika Mkutano
wa Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh,Omar Othman Makungu akielezea kuhusiana na
Siku ya Sheria Duniani ambapo kwa Zanzibar kitafanyika kilele chake
12-02-2018 katika bustani ya Victoria Mnazi mmoja mjini Unguja.Ujumbe wa
mwaka huu ni Kuimarisha Utawala wa Sheria na Kuimarisha Uchumi
Zanzibar.kushoto ni Hakimu wa Mahkama ya Ardhi Said Hemed
Baadhi
ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Jaji Mkuu wa
Zanzibar Mh,Omar Othman Makungu akielezea kuhusiana na Siku ya Sheria
Duniani ambapo kwa Zanzibar kitafanyika kilele chake 12-02-2018 katika
bustani ya Victoria Mnazi mmoja mjini Unguja.Ujumbe wa mwaka huu ni
Kuimarisha Utawala wa Sheria na Kuimarisha Uchumi Zanzibar.
Mwandishi wa Habari wa kujitegemea Mwinyimvua Nzukwi akiuliza maswali katika Mkutano
wa Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh,Omar Othman Makungu akielezea kuhusiana na
Siku ya Sheria Duniani ambapo kwa Zanzibar kitafanyika kilele chake
12-02-2018 katika bustani ya Victoria Mnazi mmoja mjini Unguja.Ujumbe wa
mwaka huu ni Kuimarisha Utawala wa Sheria na Kuimarisha Uchumi
Zanzibar.
Hakimu wa Mahkama ya Watoto Sabra Ali akitolea ufafanuzi wa baadhi ya maswali yalioulizwa katika Mkutano
wa Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh,Omar Othman Makungu akielezea kuhusiana na
Siku ya Sheria Duniani ambapo kwa Zanzibar kitafanyika kilele chake
12-02-2018 katika bustani ya Victoria Mnazi mmoja mjini Unguja.Ujumbe wa
mwaka huu ni Kuimarisha Utawala wa Sheria na Kuimarisha Uchumi
Zanzibar.
Picha na Yussuf Simai Maelezo Zanzibar
Na ali issa maelezo 5/2/2018
Jaji Mkuu wa
Zanzibar Omar Othman Makungu amesema uwendeshaji wa kesi kwa mwaka
uliomaliza hakuwa mbaya na kwa kiasi Idara ya Mahakama imefanikiwa
katika utekeleza wa majuku yake.
Hayo ameyasema
leo huko Afisini kwake Vuga mjini Zanzibar wakati akizungumza na
Wandishi wa habari kuelekea maazimisho ya wa wiki ya sheria duniani
ambayo kilele chake hufanyika February 12 ya kila mwaka.
Amesema pamoja na
changa moto zinazoikabili Idara ya Mahakama lakini wamefanikiwa
kuzitolea hukumu kesi mbalimbali ikiwemo za udhalilishaji na Madawa ya
kulevya nchini
Amesema licha ya
Wananchi wengi kulalamikia Idara hiyo kwa kushindwa kutoa hukumu kama
wanavyodai lakini changamoto kubwa inayojitokeza ni kushindwa kutoa
mashirikiano ipasavyo hasa katika kutoa ushahidi.
Jaji Makungu
amesema ni vyema Wananchi kutoa mashirikiano ipasavyo ikiwemo kutoa
ushahidi kila inavyohitajika ili kuwatia hatiani wale wanaofanya makosa
na jinai mbalimbali nchini.
“Huwezi kumtia
mtu hatiani bila kutolewa ushahidi wa kutosha..Wananchi wengi
wanashindwa kutoa ushahidi” Alisema Jaji Mkuu Makungu
Akielezea
mafanikio amesema Mahakama imefanikiwa kuyakarabati Majengo yao na kuwa
katika hali bora na hivyo kuwarahisishia Watendaji wa mahakama
kuwajibika vizuri.
Aidha alisema
wameweza kuweka vizuri Maktaba yao hali ambayo inawejengea uwezo
Wanasheria kwa kupata taluma na miongozo ya kazi kupitia Maktaba hiyo.
Akizungumzaia
kuhusu shamra shamra za maadhimisho hayo Jaji Makungu amesema
wanatarajia kufanya maonesho ya siku tatu kuazia February 9 hadi 11
katika viwanja vya maisara.
Makungu
alisema kilele cha sherehe hizo zitafanyika baraza la wakilishi la
zamani na mgeni rasmi wanatarajia atakuwa DKT. Ali muhamed shein na
Ujumbe wa mwaka huu ni kuimarisha utwala wa sheria na uchumi .