Agizo hilo amelitoa alipokuwa akiwatunuku vyeti vya kuhitimu mafunzo ya miezi mitano kwa mafundi simu 68 yaliyotolewa katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia (DIT).
Hata hivyo amewataka mafundi simu hao kutumia elimu waliyoipata katika mafunzo hayo ili waitumie kwa kuwahudumia wananchi kwa udadilifu mkubwa na kuwa mfano kwa mafundi wa aina hiyo hapa nchini.
“Kuanzisha mafunzo haya ya kurasimisha ufundi wa simu za mkononi kutawasaidia mafundi kufanya kazi kwa weledi na ufahamu lakini pia itaisaidia TCRA kutoa leseni kwa mafundi ambao kiwango chao kinafahamika”
“Yamekuja kwa wakati muafaka na naomba yaendelee kusimamiwa vyema ili mafundi simu za mikononi nchini kote waweze kupata elimu hii, ” amesema Dk Yonaz.
Aidha Dk Yonaz ametoa rai kwa wadau wa Mawasiliano nchini kubuni mipango endelevu ya kushirikiana kuchangia katika kufanikisha mafunzo hayo.