Arsene Wenger
Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amesema hajapokea mawasiliano yoyote na Real Madrid kuhusu kuziba pengo la kocha wa miamba hiyo ya Uhispania. (Bein Sport)Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino amesema inamuwia vigumu kusajili mastraika wapya katika klabu hiyo kutokana na uwepo wa nyota Harry Kane, mwenye miaka 25. (Football.London)
Paul Pogba
Kiungo wa Manchester United na timu ya taifa la Ufaransa Paul Pogba, 25, alifanyiwa vipimo vya kubaini iwapo anatumia dawa za kuongeza nguvu zinazokatazwa michezoni baada ya mechi ya United dhidi ya Juve. United ilishinda mchezo huo 2-1. Kutokana na kufanyiwa vipimo hivyo Pogba aliikosa ndege ya timu iliyokuwa inarejea Uingereza. (Manchester Evening News)
- Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 08.11.2018
- Man Utd yaishangaza Juventus nyumbani
- Fernando Ovelar
- Klabu ya Manchester City imetuma wapelelezi wake kwenda kumuangalia kinda wa miaka 14 Fernando Ovelar anayechezea klabu ya Cerro Porteno ya ligi kuu ya Paraguay. Ovelar alifunga bao la ushindi katika mechi ya mahasimu wa jadi wa ligi hiyo, na diyo mchezaji mdogo zaidi kuwahi kucheza kwenye ligi kuu ya nchi hiyo ya Amerika ya Kusini. (Mirror)Fernando Llorente
- Klabu ya Athletic Bilbao inatarajiwa kujaribu kumsajili mshambuliaji wa Tottenham raia wa Uhispania Fernando Llorente, 33, katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari. (Independent)Alberto Moreno
- Klabu ya Sevilla inamnyemelea beki wa kushoto wa Liverpool na Uhispania Alberto Moreno, ambaye kandarasi yake na Liverpool inatamatika mwisho wa msimu huu. (ESPN) Medhi Benatia
- Arsenal wanataka kumsajili beki kisiki wa Juventus na Morocco Medhi Benatia. Beki huyo mwenye miaka 31 pia anatakiwa na Manchester United.(TuttomercatoMesut Ozil
- Kiungo wa Arsenal raia wa Ujerumani Mesut Ozil, 30, ambaye amesaini kandarasi mpya na klabu hiyo ya London mpaka mwaka 2021 amesema yupo tayari kumalizia maisha yake ya soka na washika bunduki hao. (London Evening Standard) Tiemoue Bakayok
- Klabu ya Fulham inataka kumsajili kiungo wa Chelsea na Ufaransa Tiemoue Bakayoko, ambaye sasa anachezea AC Milan kwa mkopo. Kiungo huyo mwenye miaka 24 amecheza mechi mbili tu na Milan na tayari ameshakosolewa na kocha wa klabu hiyo Gennaro Gattuso. (Calciomercato, via Sun)
- FA waamua hawamwachi Mourinho
- Callum Wilson
- Mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson anawindwa na Chelsea ambao wapo tayari kutoa £35 milioni kumsajili. Straika huyo mwenye miaka 26 aliitwa kuchezea timu ya taifa ya England kwa mara ya kwanza siku ya Alhamisi. (Sun)