Watu watatu wamefariki Dunia na wengine kumi na saba wamelazwa katika hospitali ya Mnazi mmoja baada ya Gari aina ya Double Coaster kupata ajali katika kijiji cha Muyuni wilaya ya Kusini Unguja kiasi cha maili 30 kutoka mjini Unguja.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna Msaidizi wa polisi Suleiman Hassan Suleiman, tukio hilo limetokea jana majira ya saa kumi na moja na nusu jioni. Kamanda Suleiman amewataja waliofariki ni kuwa Dorice David miaka 28 mkazi wa Kijito Upele, Neema Paul Jembe miaka 24 mkazi wa Mpendae na Masoud Khamis Msabah miaka 28 mkazi wa Tomondo ambaye alifariki njiani kabla ya kufikishwa hospitali Kuu ya Mnazi mmoja.
Kamanda Suleiman amesema ajali hiyo imetokea baada ya Gari yenye namba za usajili Z 285 JJ iliyokua imepakia wa Wafanyakazi wa Reidence iliyoko Mchangamle Kizimkazi ikielekea mjini ikiendeshwa na Ndugu Wadi Hassan Ali mkaazi wa Bububu kuacha njia na kugonga Mnazi.
Kamanda Suleiman amesema Dereva wa gari hiyo kwa sasa anashikiliwa na polisi kwa hatua za kisheria