Imeandikwa na Khadija Mahmoud , Pemba
WANAFUNZI wa kidato cha sita wa skuli yamchangamdogo wametakiwa kushughulikia masomo yao badala ya kujihusisha na vishawishi vibaya vinavyopelekea kutofanya vizuri katika mitihani yao.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Utumishi Wilaya ya Wete Faki Hamad Faki wakati akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo huko katika Skuli ya Sekondar Mchanga Mdogo katika Maafali ya tano ya kuwaaga wanafunzi wanaotarajiwa kumaliza masomo yao ya kidato cha sita hivi karibuni.
Amesema Vijana ndio nguvu kazi inayotegemewa na Taifa hivyo ni vyema kutumia muda wao vizuri katika kujitafutia elimu huku wakijiepusha na vikundi viovu.
Aidha amesema watakapojiingiza katika mambo ambayo sio mazuri kwao watashindwa kufanya vizuri katika mitihani yao ya kumalizia masomo.
Mapema mwalim Mkuu wa skuli hiyo Juma Said Hamad amesema Skuli hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya uhaba wa vikaliwa pamoja na walimu wa kufundisha masomo ya sanyansi hivyo kupelekea wanafunzi kushindwa kufanya vizuri katika masomo hayo.
Akizungumza kwa niaba ya wazazi Juma Sleiman Juma amewataka wazazi kushirikiana na kamati ya skuli pamoja na walimu ili kuhakikisha wanawasimamia vyema wanafunzi katika masomo yao na kuwashauri vijana wale ambao hawatafaulu katika mitihani yao wajiendeleze katika vyuo vya amali ili waweze kupata ujuzi kupitia vyuo hivyo.