Mvuvi mwenye umri wa miaka 20 amefariki akiwa baharini akiwa katika harakatia za kutenga chombo huko Pwani ya kibuyuni Wilaya ya Kusini Unguja.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa kabla ya kifo chake marehrmu huyo alikuwa akirudi baharini kutenga chombo katika harakati za kuogelea wakati akirudia ndipo alipozama naharakati za kumtafuta kwa mashuhuda watukio hilo zilianza kuanzia saa 10 za jioni hadi saa 2 za usiku ndipo alipo kutwa ufukweni akiwa ameshafariki.
Sheha wa shehia ya Muyuni A Mauli Hassan Zidi ameeleza kuwa waliposikia taarifa yakuzama kwa marehemu huyo ndipo walipoamua kueka dago katika sehemu hiyo nakuanza harakati za kumtafuta.
Ameendelea kwa kusema kuwa baada ya maji kukupwa ndipo walipofanikiwa kumuona sehemu ileile aliozama akiwa ametulia lakin tayari ameshafariki.
Sheha huyo ametoa wito kwa Askari wauokozi kuwa makini wakati wanaposikia taatifa kama hizo ili kuepusha kutokea kwa athari kama hizo.
Kwaupande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi Makarani Khamis Ahmed amewaomba wavuvi wawe na tahadhari wanapokuwa katika harakati zao za uvuvi ili kuepuka athari kujitokeza.