Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Makamu wa Rais (Sera na Uratibu), Profesa
Faustine Kamuzora (kulia), na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango, Amina Khamisi Shaaban, wakisaini hati za makabidhiano ya sh.
trioni moja zilizotolewa na Shirika la Global Fund kwa Serikali ya
Tanzania kwa ajili ya kusaidia mapambano ya Ukimwi, TB na Malaria katika
hafla iliyofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam leo.
Wengine waliosimama katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na viongozi wengine kutoka Global
Fund.
Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania, Frederic Clavier, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mnufaika wa Global Fund, Joan akielezea jinsi alivyo nufaika na shirika hilo.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaishi na VVU-Ukimwi, Mwinuka Juastine, akizungumza.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamisi Shaaban (kulia),
akimkabidhi hati ya makabidhiano Mwakilishi wa Global Fund Tanzania,
Linden Morrison.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Makamu wa Rais (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora, akizungumza.
Taswira ya ukumbi wa mkutano katika uzinduzi huo.
Na Dotto Mwaibale
SHIRIKA
la Kimataifa la Global Fund limetoa shilingi trioni moja kwa Serikali
ya Tanzania kwa ajili ya mapambano ya magonjwa ya ukimwi, malaria na
kifua kikuu kwa mwaka 2018-2020.
Akizungumza
katika hafla ya kutiliana saini makabidhiano ya fedha hizo baina ya
mfuko huo na serikali Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Ummy Mwalimu alisema fedha hizo ni muhimu sana kwa nchi yetu.
Alisema
fedha hizo zitaelekezwa katika kupambana na magonjwa hayo ambapo kwa
ugonjwa wa ukimwi zimetolewa sh.bilioni 769, TB sh. bilioni 67 wakati
malaria sh.bilioni 320.
Alisema
fedha hizo zitatumika kikamilifu kwa lengo lililokusudiwa na
zitasimamiwa na Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Afya na Mashirika Yasiyo ya
kiserikali.
Alisema
katika masuala ya ukimwi zitatumika kwa ajili ya vipimo, dawa za
kurefusha maisha na kufubaza virusi kwa wagonjwa wa ukimwi na katika
ugonjwa wa malaria fedha hizo zitatumika kwa ajili ya vipimo na matibabu
pamoja na kununua vyandarua.
"Kwa
upande wa wagonjwa wa TB ni asilimia 40 tu ndio waliofika kwenye vituo
vya afya na kuthibitika kuwa na maambukizi na wamepatiwa matibabu lakini
tunataka hadi ifikapo mwaka 2020 tunataka asilimia 70 ya watanzania
watakaogundulika kuwa na maambukizi wajulikane na wapatiwe matibabu"
alisema Ummy.
Ummy
aliongeza kuwa kati ya wagonjwa 100 wenye maambukizi ya TB wagonjwa 90
waliothibitika kuwa na maambukizi walitibiwa na kupona kabisa.
Katika
hatua nyingine Waziri Ummy amewataka Katibu Mkuu wa Wizara yake,
Tamisemi na Ofisi ya Rais kuhakikisha wanazisimamia vizuri fedha hizo
ili kupata matokeo mazuri waliyo yakusudia.
Mratibu
wa Watu Wanaotumia Dawa za Kulevya Tanzania (TANPUD), Happy Assan
alisema mradi huo utawasaidia sana na kuhakikisha hawataathirika
ukizingatia kuwa fedha hizo zitawafikia walengwa.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaishi na
VVU-Ukimwi, Mwinuka Juastine alisema mradi Global Fund imewasaidia
waathirika 900,000 kwa kuwapa dawa za kupunguza makali ya ukimwi ARV na
kufubaza virusi vya ugonjwa huo.