Simba ina mwendo wa kimondo kutokana na kufanikiwa kushinda mfululizo.
Katika mechi tatu, imekusanya pointi 12
na mabao 12 ukiwa ni wastani wa juu kabisa wa Ligi Kuu Bara. Lakini
Masau Bwire anasema, wakati wa ukombozi kwao umfika.
Bwire anasema, umefika wakati wa
kuisimamisha Simba ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja na wajue ndiyo
ule wakati wa kulipa kisasi.
Katika mzungumzo wa kwanza wa Ligi Kuu
Bara, Simba ilitwanga Shooting kwa mabao 7-0. Lakini Bwire anawaambia
Simba, Ruvu Shooting hii si ile. Hivyo mechi ijayo, watarajie kipigo.
“Tuna morali ya kutosha kwa sasa, hasa
baada ya kufanya vizuri kwenye mechi yetu iliyopita dhidi ya Mbao FC, na
sasa tunaelekeza nguvu zetu kwenye mchezo ujao dhidi ya Simba ambao
tumewapania kuwaonyesha kwamba kwa sasa ni bora tofauti na mwanzo ambapo
walitufunga mabao 7-0.
“Tunataka kulipiza kisasi kwa wakati huu
na hilo linawezekana kwa sababu kocha Abdulmutik Haji anaendelea
kuwanoa vijana ili waweze kufanya makubwa kwenye mchezo huo, hao Simba
wajipange kwelikweli kwa sababu tunataka kufanya vizuri kwa sasa ili
kubakia kwenye ligi kwa msimu ujao,” alisema Bwire.