Ikiwa
ni siku chache baada ya kupoteza mechi yake ya Ligi Kuu Bara dhidi ya
Yanga, Azam FC imeibukia katika michuano ya Kombe la Shirikisho na kutoa
adhabu kali.
Timu
hiyo, ilivana na Shupavu inayoshiriki Ligi Daraja la Pili katika mchezo
huo uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Katika
mechi hiyo shujaa wa mchezo huo ni kinda, Paul Peter wa Azam ambaye
alipiga ‘hat trick’ katika mechi hiyo katika ushindi wa mabao 5-0.
Katika mchezo huo Azam ilionekana kumiliki mpira vyema katika vipindi vyote viwili huku bao la kwanza kwenye mchezo huo likifungwa dk 45 ya mchezo huku la pili likafungwa dakika hiyohiyo baada ya kuongezwa dakika mbili.
Peter alifunga mabao katika kipindi cha pili cha mchezo huo akifunga dakika ya 57, 77 na 88 huku timu yake ikitangulia katika hatua hiyo ya 16 bora.
Mabao
mengi ya timu hiyo yalifungwa na Yahya Zaydi katika dakika ya 45 kwa
njia ya penalti kabla ya Iddi Kipagulile kumchabua kipa wa Shupavu
katika dakika za nyingeza baada ya kuwatoka mabeki wa timu hiyo.