
Msafara wa watu zaidi ya 30 wakiwemo wachezaji 21, kesho Alfajiri unatarajiwa kuondoka kwenda Eswatini, huku John Bocco na Meddie Kagere wakitamba lazima washinde.
Mbabane Swallows itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa Jumanne ijayo kwenye Uwanja wa Mavuso Sport Center. Katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar, Simba ilishinda mabao 4-1.
Hata hivyo, kabla ya Simba kuondoka kesho, tayari Simba ilimtuma mratibu wake, Abassi Ally kwenda kuweka mazingira sawa kabla ya timu kuwasili hiyo kesho Jumapili.
Mkuu wa Kitego cha Mawasiliano cha Simba, Haji Manara alisema, msafara huo utaondoka na Shirika la Ndege la Ethiopia na wanatarajiwa kufika siku hiyohiyo.