
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi habari, ambapo amedai kuwa kuna viongozi wenzake ambao ni vijana wamekuwa wakimuangusha kwa kuwa wana mamlaka.
“Nimesoma twiti za Kigwangala, mimi nasema yule ni mchumia tumbo anashindwa kutambua kuna wazee wamenifuata kulalamika hawajalipwa mafao kwa miaka 2, anataka tuamini kuwa yale ndiyo maoni ya Baraza la Mawaziri, asisahau hata yeye aliendesha mgomo wa madaktari alivyokuwa Daktari Muhimbili,”amesema Bulaya
Aidha, wakati huo huo Bulaya amemshukuru Spika Job Ndugai kwa kile alichokieleza kuwa amempongeza juu ya msimamo wake kuhusu suala ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii.